Basata: Kashfa ya Sitti mikononi mwa RITA

Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa(Basata), imetoa tamko kuhusu kashfa ya kugushi cheti kwa aliyekuwa Miss Tanzania Sitti Mtemvu, ikieleza kuwa kwa sasa suala hilo lipo chini ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Tamko hilo la Serikali limekuja wiki moja tangu mrembo huyo alipovua taji hilo na kulikabidhi kwa waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Kampuni ya Lino Agency chini ya mkurugenzi wake Hasheem Lundenga.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema kuwa Serikali imekamilisha kazi yake, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa urembo nchini na kwamba suala la kughushi lipo mikononi mwa Rita.

Alisema kwa sasa sheria inayotakiwa kutumika dhidi ya Sitti Mtemvu kuwa siyo ya Basata bali ya masuala nyeti yanayohusu sekta nyingine tofauti.

Kanuni za kuendesha Mashindano ya Miss Tanzania zinajulikana, mara lilipotokea tatizo tulimweleza Lundenga kwamba anatakiwa kufuata sheria zinavyosema. Kama Serikali kupitia Basata tumefanya kazi yetu, suala limebaki mikononi mwa Rita kwani jukumu letu ni kuhakikisha kanuni zilizowekwa zimefuatwa,” alisema Mngereza.

Alisema kuwa upande wa kanuni na vigezo vya Miss Tanzania vinaeleza wazi kwamba mrembo akiwa amekiuka moja ya kanuni zilizopo, atavuliwa taji kwa mujibu wa mwongozo kwa kuwa wao ndiyo wanaosimamia suala hilo ikiwamo kuchagua majaji.

Hatukuwa na sababu za kumbana Sitti Mtemvu katika hili, sheria zinasema kwamba sisi tulitakiwa kuwasiliana moja kwa moja na yule tuliyempa leseni ya kuendesha mashindano haya (Miss Tanzania), ndiyo maana tulihitaji awajibishwe.

Lundenga aliiomba wizara iunde tume

Mngereza alibainisha kuwa hata baada ya kuibuka vurumai hiyo lililoacha historia isiyovutia kwa waandaaji wa Miss Tanzania, Lundenga aliiomba Basata kuwapa mwongozo na wao walimtaka arudi kujieleza kwa vyombo vya habari.

Mngereza alifafanua kuwa baada ya kuona hali inakuwa mbaya, Lundenga aliiomba wizara iunde tume kuchunguza sakata hilo na kwa kuwa wao ndiyo waliotoa leseni ya kuendesha mashindano hayo walilivalia njuga.

Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Juma Nkamia alisema, wizara nyake imeshamaliza suala hilo na kwa kuwa yeye bado yupo safarini, Basata walikuwa wakilishughulikia.

Suala hili lilikuwa mikononi mwa Basata, baraza hilo linatoa kibali au leseni ya kuendesha mashindano, suala la kutoa vyeti vya kuzaliwa lipo chini ya Rita, wao wanatakiwa kuchukua hatua kuhusu hili,” alisema Nkamia.

Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s