Picha: Omary Abdallah awa bingwa wa kutunisha misuli kwenye shindano la Body Building Champions 2014

Wadau na viongozi wa TBBF wakiwa na washindi wanne wa mashindano hayo.

MCHEZO wa utunishaji misuli unaonekana kusahaulika sana katika jamii ya Kitanzania , lakini ni mmoja kati ya michezo mizuri na yenye kufurahisha  kwa watazamaji.

GPL ilishuhudia zaidi ya washiriki 10 wakimenyana vikali katika shindano la kumsaka mtunisha misuli lililopewa jina la Body Building Champions 2014, uliofanyika katika Ukumbi wa Sunsiro, Sinza,  jijini Dar es Salaam, ambapo Omary Abdallah kutoka Mbeya ndiye aliyeibuka kidedea na kujishindia zawadi ya shilingi  500,000/= pamoja na ‘rise cooker’, huku mshindi wa pili akijinyakulia 300,000/= pamoja na ‘blenda’, mshindi wa tatu nayeye aliondoka na 200,000/= na pasi ya umeme, huku mshindi wa nne akipata 200,000/=, pamoja na medali za ushiriki kwa washindi  wote wanne, huku washiriki wote wakipata kikaangio cha chapatti ‘frying pen’,  na vyeti vya ushiriki.

Aidha wadau wa mashindano hayo wakiwemo Tanzania Body Building Federation ‘TBBF’ wamewaomba wadau kujitokeza kwa wingi ili kuukuza mchezo huo, kwani unajenga afya ya mchezaji lakini pia ni biashara kwa washiriki.Kujua mengi tembelea

Omary Abdallah, mshindi wa Body Building Champions 2014.

Mshindi wa pili, Erick Majura akiwa katika pozi.

Kushoto Erick Majura  mshindi wa pili (Mwenye kaptula nyeusi), mshindi wa kwanza Omary Abdallah wakiwa na wadau wa mchezo huo.

Credit GPL.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s