Joyce Kiria akwaa skendo ya utapeli

 Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria

Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya Telexfree Network Marketing.

Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote.

Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: Ni kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.
Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”

Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.

Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s