Kuhusiana na Mmasai aliyepeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi wa Wema

Habari mpya kutoka kwa mlimbwende asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam au Beautiful Onyinye’ ni kwamba, Mmasai wa Kigoma, Ayoub Nyembo ‘Masai’ ameibuka na kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini DarHabari mpya kutoka kwa mlimbwende asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam au Beautiful Onyinye’ ni kwamba, Mmasai wa Kigoma, Ayoub Nyembo ‘Masai’ ameibuka na kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar

Mtu wa karibu na Masai alilipenyezea gazeti hili habari kuwa, baada ya habari za Wema kummwaga mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuandikwa magazetini hivi karibuni, fasta Masai aliiona fursa ‘u-single’ kwa Wema, akatangaza nia ya kumposa kwani alikuwa akimzimia muda mrefu.

Masai ametumia fursa, hakutaka kuchelewa maana wazo alikuwa nalo kitambo lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kumhofia Diamond,” alisema mtu huyo.

Baada ya mtu huyo wa karibu na Masai kupata mawasiliano ya Ijumaa Wikienda kisha alikutanishwa nalo maeneo ya Mwenge jijini Dar akiwa tayari ‘amejikoki’, mkononi akiwa na barua ya uchumba sambamba na bahasha yenye shilingi elfu hamsini kama posa.

Ijumaa Wikienda: Unataka kumuoa Wema kweli au unazingua?
Masai: Nipo ‘serious’ ndiyo maana unaona nimekuja kwako nikiwa kamili na mshenga wangu nipeleke kwa mama Wema.

Huku mwanahabari wetu akigonga picha za kumwaga kwa kila hatua, alimwelekeza Masai huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva nyumbani kwa mama Wema, Mariam Sepetu ‘Mkwe’ ambapo waliambatana na mshenga wake lakini walipokaribia, Masai alikaa sehemu na kumtuma mshenga azame ndani.

Mshenga alipozama ndani, alikutana na mfanyakazi wa ndani (house girl) ambaye alipokea barua hiyo ya uchumba na kumpelekea moja kwa moja mama Wema.

Baada ya kutua mikononi mwa mama Wema, aliisoma barua ya uchumba kisha akamuomba mshenga kuingia ndani huku akiwa na furaha hususan pale alipogundua kuwa mkwewe mtarajiwa (Masai) ni mtu wa Kigoma.

Kwa hiyo Wema wangu anatakiwa aolewe Kigoma akale migebuka eeh?,” mama alimuuliza mshenga.

Bila hiyana mshenga akajibu: “Ndiyo mama, Masai anaishi Kigoma ila ana nyumba zake Dar, huwa anakuja mara kwa mara kwenye biashara zake na pia ana mji Singida katika Kijiji cha Ikungi na ni mfugaji mzuri, ng’ombe anao wa kutosha.”

Shangwe zaidi iliongezeka kwa mama Wema baada ya kusikia Masai huyo ana mji Singida tena kwenye kijiji ambacho yeye anatokea akatoa masharti kuwa afuate taratibu za Kitanzania kwa kumtaka Masai azungumze na Wema kisha ampigie simu ndiyo apokee barua kwa amani.

Hili ni jambo la kheri jamani, nimekuelewa lakini uchukue barua hii sambamba na posa urudi kwanza ukamwambie huyo mkwe mtarajiwa azungumze na Wema wakikubaliana, Wema yeye ndiye aniambie siku ya ninyi kuja kutoa posa ili na mimi nijiandae,” alisema mama Wema.

 Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s