Beef ya Diamond na Q Chief yaisha, Diamond kufanya naye audio na video

Kama ni mfatiliaji mzuri wa muziki na wasanii wetu utakumbuka kuwepo kwa bif kubwa kati ya Diamond na mkongwe Q chief baada ya Q kudai kuwa Diamond anatembelea nyota yake (anamloga).

Good news ni kwamba bif hilo limekwisha na Diamond amempa ofa ya kumlipia Q chief audio pamoja na video ili atusue maana ni msanii ambae anaemkubali.

Q Chief namkubali sana, anajua sana kuimba, ana miziki ambayo watanzania wanaipenda sana lakini sifaham tatizo ni nini siwezi kujaji, lakini sikuzote natamani, kuna kipindi lani nishawahi nilikua nipo na prof jay nakumbuka nilikuwa niko uingereza nikamwambia ukikutana nae zungumza nae mwambie mi ntamlipia video na audio akashoot akafanye ngoma ambayo naamini atatusua, lakini bahati mbaya sijui ikawaje kawaje ikaishia hivyo.Ni mtu ambae natamanigi nisikie ngoma zake kila dakika….” amesema Diamond

Sikiliza:

Q chief nae alikuwa na haya ya kusema

Mimi nataka nikwambie kitu kimoja, Diamond ni mdogo wangu ambae nampenda, napenda mziki wake, halafu hakuna msanii katika historia hii ambae amefika hata MTV au BET, yule mtoto amenishangaza amefika ni kwamba mimi mwenyewe am inspired by him, nikwamba wakati mimi namzungumzia yeye  nyinyi mlikuwa hamuelewi, nasema ukweli kwamba Diamond ni msanii wa kuigwa hata Alikiba nae alipata nafasi lakini pamoja na kwamba anarudi anafanya vizuri lakini anahitaji kufanya nae kazi na mi nahitaji kufanya nae kazi. Diamond ni msanii wa kuigwa, mi staki matatizo na Diamond i ove him i like him as a brother, kwahiyo mi nampenda yul dogo…” amesema Q Chief. 

Credit DJFetty

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s