Exclusive: Undani wa maisha ya Hemedy PHD, fahamu kinachomlipa zaidi kati ya filamu na muziki

Ukiikwepa sauti ya Hemedy PHD kwenye redio, basi huenda ukashindwa kuikwepa sura yake kwenye video za muziki au katika filamu mbalimbali za Tanzania.

Kwa miaka mingi, muimbaji huyo aliyegeuka kuwa muigizaji wa filamu na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, ameendelea na harakati kwenye fani hizo mbili kwa speed isiyo na dalili ya kupungua.
Bongo5 imezungumza na Hemedy kutaka kujua maisha ya muziki na filamu yanaendaje kwa sasa.

Hemedy anakiri kuwa filamu zinamsaidia kwa kiasi kikubwa kumpa vitu vingi anavyohitaji katika maisha yake licha ya kukiri kuwa muziki anaupenda zaidi. Hata hivyo kwenye muziki, staa huyo ameonekana kuwekeza nguvu zake nyingi kwenye kufanya video kuliko kusimamia promotion ya audio kwenye redio.

“Video zimefanya track zangu zijulikane kuliko audio,” anasema. “Na hii nataka kuiendeleza sababu katika maisha ya entertainment nilizaliwa kwenye TV. Kuanzia Project Fame ilikuwa ni TV, kwenye movie japo haimaanishi kuwa nitaacha kurelease audio lakini nimegundua kuwa ngoma zangu hazipati airplay kwenye audio. Lakini video ikitoka kunakuwa na impact kubwa.”

Kwa upande wa filamu, Hemedy anada kuwa filamu nyingi zinazomuingizia kipato kikubwa ni zile ambazo amefanya na watayarishaji wapya kwenye industry. “Hizi filamu mpya zinazofanywa na maproducer wapya, ndizo huwa filamu zinazolipa fedha nyingi sana tofauti na unapoitwa na msanii mwenzako au na mtu ambaye umezoea kufanya naye kazi,” anasema.

Anadai kuwa pamoja na kuwapa fedha nyingi, watayarishaji wapya huwa na kasumba ya kuwajali zaidi wasanii ingawa anakubali kuwa ni sahihi kufanya bei ya kishkaji kwa wasanii anaofahamiana nao ambao mwisho wa siku nao huwa na msaada kwake.

“It’s also fair sababu unaweza kukwama sokoni mhindi akakuambia namhitaji mtu fulani halafu ukizingatia ulimkazia inakuwa haileti maana, japo wengine hawafanyi hivyo, wengine wanakaza.”
Pamoja na kutoitaja filamu iliyomuingizia mkwanja mrefu zaidi, Hemedy amedai kuwa mara nyingi amekuwa akilipwa bei aliyojiwekea kama thamani yake anapoitwa kufanya movie.

“Huwa nina bei yangu fulani ambayo naweza kusema kwa kiasi kikubwa filamu ambazo nimefanya mwaka huu wengi walifika pale.”

Hemedy amesema filamu zinamsaidia kumpa uwezo wa kuendelea muziki wake hasa pale anapokwama.

“Imeshawahi kutokea mimi nimeenda show Sengerema, naperform nashuka, nakuta promoter ameondoka pesa yangu hajanilipa, tiketi ya ndege haijawa confirmed. Kwahiyo mwisho wa siku unaamua unachomoa fedha ambayo ipo kwenye filamu, unachukua ndege, unalipa hoteli, unatulia. Sengerema mpaka Mwanza, pengine usafiri almost laki moja ukitumia gari private sababu huwezi kupanda mabasi haya. Kwahiyo kuna vitu vingi vinatokea upande wa pili uwa unacover. But at the same time hata huu upande mwingine unacover. Kwa mfano kipindi hiki almost miezi mitatu nimekuwa niko busy sana kufanya show za mikoani ambako naingiza fedha nyingi kupitia muziki, kwahiyo vinategemeana. Lakini filamu inaplay role kubwa sana kunisaidia vitu vingi.”

Katika hatua nyingine, msanii huyo anaamini kuwa ni ngumu kwa asili ya soko la filamu Tanzaia msanii kama yeye kupata connection ya kufanya filamu za kimataifa kama yeye mwenyewe hajazunguka kutafuta.

“Kwa jinsi ilivyo sasa hivi ni wewe kuiendea, sio wao kukutafuta. Kwa jinsi soko letu lilivyo unatakiwa wewe utoke, utume profile yako zako wakuone, pengine wakuchague uweze kushiriki kwenye project zao kubwa which is my wish.”

Tofauti na wasanii wengi, Hemedy anadai kuwa tamanio lake kubwa ni kuingia kwenye soko la filamu la Afrika Kusini kuliko Nigeria.

“Focus yangu kubwa ipo kwenye industry ya South Africa na wala sifikirii industry ya Nigeria kabisa au Ghana. Nimegundua South Africa kuanzia quality, quantity na kila kitu wana uwezekano mkubwa wa kupenya ya kwenda Hollywood. Soko la South Africa ndio ambalo mimi huwa linaniumiza kichwa and I wish one day niweze kushiriki filamu zao.”

Hata hivyo pamoja na kuwa na filamu nyingi sokoni, Hemedy si mtazamaji mzuri wa filamu zake na hata zingine za Kibongo.

“Mimi binafsi huwa sitizami filamu za kibongo, unless inikute sehemu halafu nipo, lakini najua sitaimaliza,” anasema. “Binafsi mimi kama Hemedy, sijawahi nikakaa nikatizama movie yangu hadi mwisho, haijawahi kutokea.”

Anadai kuwa anachofanya ni kupokea tu maoni kupitia mitandao ya kijamii kutoka kwa watu waliotazama ambao humweleza walichofurahishwa au kuchukizwa kwenye filamu zake na kufanyia kazi maoni hayo.

“Japo ninachokifanya sio kizuri kwasababu kama msanii nilipaswa nijitizame lakini nakuwa tu napoteza interest. Kwasababu interest yangu ipo zaidi kwenye muziki kuliko filamu.”
Jacqueline Wolper na Irene Uwoya ni wasanii maarufu wa kike aliowahi kuigiza nao lakini ni nani anayependa kufanya naye zaidi kazi?

“Wote huwa naenjoy nao lakini Wolper amekuwa mtu wangu wa karibu sababu nimefanya naye kazi nyingi,” anasema. “Irene ni mtu ambaye namheshimu lakini hatuna mazoea yale ya kihivyo. Kwanza katika wasanii wote wa kike, nafikiri ndio msanii wa mwisho kufanya naye, kwahiyo mazoea kidogo sio sana japo tuko vizuri sana, we hang out. Wolper nimemzoea sana sababu nimefanya naye movie nyingi mno, ni mshkaji, nakuwa comfortable sana na Wolper, lakini wote nakubali sanaa zao.”

Credit Bongo5

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s