Rich Mavoko azitaja silaha mpya za kufungia mwaka

Baada ya kuachia ‘Pacha Wangu’, Rich Mavoko amesema yupo chimbo kuandaa silaha za kufunga mwaka.

Mavoko ameiambia Bongo5 kuwa sababu inayomfanya aachie wimbo mpya ni baada ya kuona mashabiki wa muziki wake bado wanahitaji mawe zaidi kutoka kwake.

“Kuna kazi ipo ndani imeshafanyiwa kila kitu, manejimenti wapo kwenye maandalizi kwaajili ya uzinduzi. Mimi nahisi inaweza ikatoka kufunga mwaka na pia kama tukiona vipi inaweza ikatoka kufungulia mwaka.” amesema Mavoko.

Katika hatua nyingine Mavoko amesema mwaka huu umekuwa wa neema zaidi kwake.

“Mwaka huu umekuwa vizuri sana kwenye biasahara ya muziki wangu, kwahiyo tunajipanga na kuomba Mungu mwakani uwe mzuri zaidi. Kuna mambo makubwa nimeyafanya mwaka huu lakini siwezi kuyaweka hadharani bado haijaisha. Lakini mambo yako vizuri, vikiisha watu wataviona.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s