Chanjo ya Ebola yaonesha matumaini

Wanasayansi wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema dawa zinaonesha kuwa salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua virusi hivyo.
Watu 20 waliojitolea kutoka nchini Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.

Utafiti wa chanjo hiyo ya ebola kama huenda ikaokoa maisha wa maelfu walio hatarini kuambukizwa virusi hivyo. Dr Anton Fauci ni mkuu wa Taasisi ya Marekani ya magonjwa ya kuambukiza :
“Kwa upande wa usalama na uwezo wa kuleta matokeo mazuri nadhani tunaweza kuita majaribio haya ya chanjo haikufanikiwa. Japokuwa katika mkondo wa awali imeonyesha mafanikio makubwa.” Amesema Fauci

Hata hivyo watafiti wanasema matokeo hayo sio uthibisho kwamba chanjo hiyo inafanya kazi lakini kama majaribio ya awali yamekuwa na mafanikio basi chanjo ya eboal itatolewa kwa maelfu ya wafanyakazi wa afya huko Afrika Magharibi kuanzia mwezi Januari mwakani.

Zaidi ya watu elfu tano mia tano wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya ebola.Kwa sasa chanjo imekuwa ikifanyiwa utafiti na kampuni GlaxoSmithKline.

Dr Colin Brown ni mtaalamu wa magonjwa ambaye amepokea habari za chanjo hiiyo kama habari njema.

“Kwa vile suala la usalama limepewa umuhimu tunayo furaha kwamba hakuna madhara yaliyotokana na chanjo. Ambapo imeonyesha wagonjwa wa awali wapatao 20 wakuwa na tatizo lolote. Ninadhani tutarajie kuona itasaidia hasa kwa upande wa wafanyakazi wa afya kujilinda wakiwa kazini. ” Alisema Bwana Brown

Credit BBC

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s