Picha: Kutana na Gabby, mtoto wa miaka 9 atakayekuwa mtoto maisha yake yote bila kuwa mkubwa

Gabby Williams ana uzito wa kilo 5 – zaidi kidogo tu ya mtoto mchanga. Ana sura ya kichanga na anavaa nepi. Lakini Gabby ana miaka tisa.

Tangia azaliwe ameendelea kuwa hivyo hivyo.

Gabby ana tatizo nadra ambalo bado halijapewa jina. Amekuwa akipewa jina la utani la Benjamin Button wa ukweli, sababu kama kwenye filamu hiyo ya Brad Pitt, Gabby ana tatizo ambalo linaathiri mchakato wa ukuaji.

Humchukua miaka minne kukua kama mwaka mmoja.

Gabby anaishi Marekani na wazazi wake pamoja na ndugu zake watano. Ni mtoto wa pili kuzaliwa lakini mdogo kuliko wote kwa muonekano.

Gabby alizaliwa kipofu na hawezi kuongea. ‘Hulia anapoumia na wakati mwingine hutabasamu,’ anasema mama yake.

Pamoja na kuwa na miaka 9, Gabby bado anaishi kama mtoto mchanga kwa kunywesha maziwa kwa chupa kila baada ya masaa matatu na anahitaji kuangaliwa mara kwa mara.

Miaka michache iliyopita, familia ya mtoto huyo iliamua kujitangaza ili kujua zaidi kuhusiana na tatizo hilo. Tangu hapo wamegundua kesi mbili za aina hiyo.

Moja ni ya mwanaume mwenye miaka 29 wa Florida lakini mwenye umbo kama la mtoto wa miaka 10. Mwingine ni mwanamke wa Brazil anayeonekana kama mtoto anayeanza kutembea lakini ana miaka 31.

Kama Gabby, hakuna maelezo ya kwanini watu hao wanakua taratibu kuliko watu wengine.

Chanzo: Daily Mirror

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s