Sehemu ya pili: Fahamu hapa kuhusu shinikizo la damu la juu (Hypertension)

Soma hapa Sehemu ya kwanza: Fahamu hapa kuhusu shinikizo la damu la juu (Hypertension)

SABABU ZA KUPANDA SHINIKIZO LA DAMU
Shinikizo la damu hupanda wakati damu nyingi inapopita mshipani au wakati mshipa unapokuwa mwembamba.
Mtu anaweza kupata ugonjwa huu kwa mambo yasiweza kuepukika na mambo yanayoweza kuepukika.

Mambo yasiyoweza kuepukika mfano kurithi tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu kupitia kuzaliwa pamoja kwenye familia yenye watu wenye shinikizo la damu la juu.

Pia inasemekana kwamba uwezekano wa kupata tatizo hilo huongezeka mtu anapozidi kuzeeka na kwamba wanaume wenye asili ya afrika wanakabili uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo.

Mambo unayoweza kuepuka ni pamoja na matumizi ya chumvi (Sodium). Hii inahusu hasa wagonjwa wa kisukari, watu ambao shinikizo la damu hupanda sana, wazee na watu fulani weusi.

Mafuta mengi katika damu yanaweza kufanyiza utando wa kolesteroli (Cholesterol) kwenye kuta za ndani za mishipa. Hivyo, mishipa huwa myembamba na shinikizo la damu huongezeka.
Watu ambao ni wazito kupita kiasi kwa asilimia 30 wanaweza kupata tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.

Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha utando mgumu wa mafuta kwenye kuta za mishipa, ugonjwa wa kisukari, mshtuko wa moyo na kiharusi.

Ijapokuwa uthibitisho unapingana, kafeini inayopatikana katika kahawa, chai na vinywaji vya kola yaweza kusababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.
Kunywa kileo mara nyingi na kupita kiasi na kutofanya mazoezi kwaweza kuongeza shinikizo la damu.

DALILI NA ISHARA (SYMPTOMS & SIGNS) ZA KUPANDA SHINIKIZO LA DAMU
Mara nyingi watu wenye shinikizo la damu la juu hawana dalili za moja kwa moja na huwa inagundulika baada ya kufanya uchunguzi kwa kawaida au wakati maangalizi ya afya yanafanywa kwa sababu nyingine.

Watu wengine wenye shinikizo la damu la juu huwa wanapata maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi), pamoja na kuchanganyikiwa, kizunguzungu, kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni), kutoweza kuona vizuri au matukio ya kuzirai.

KUJUA KAMA SHINIKIZO LA DAMU LIMEPANDA
Pale mtu anapokuwa na dalili za kupanda kwa shinikizo la damu, hupaswa kufika kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kama shinikizo la damu limepanda.
Vipimo vya shinikizo la damu vinapatikana katika vituo vya afya na wajuzi mbalimbali wa afya wanaweza kuvitumia.
Kipimo kimoja cha shinikizo la damu hakimaanishi kupatikana au kuugua ugonjwa huo, inanidi kupimwa zaidi ya mara mbili kwa nyakati tofauti. Kama shinikizo lako la damu liko juu, ni muhimu kufanyiwa uchunguzi zaidi wa matatizo mengine ya kiafya.

Vipimo vingine ni pamoja na kuchunguza damu ili kufahamu wingi wa kolesteroli (Cholesterol) mwilini, kupimwa BUN na electrolytes, kuchunguza mkojo (Urinalysis), ECG, Echocardiography na pia ultrasound ya figo.

JINSI YA KUISHI NA SHINIKIZO LA DAMU LA JUU
Mabadiriko ya maisha hupendekezwa ili kushusha shinikizo la damu lililopanda kabla ya kuanza matumizi ya dawa za tiba (Antihypertensives).

1.  Kudumisha uzito wa mwili wa kawaida. Kwa mfano Mwili Molekuli Index (BMI) ya 20-25 kg/m°2
2.  Kupunguza kiasi cha chumvi (Sodium) unachotumia. Kupunguza ulaji wa sodium kwa < 100 mmol/siku (<6g ya kloridi sodium au < 2.4 g ya sodium kwa siku).
3. Kufanya mazoezi kwa ukawaida. Kushiriki katika shughuli za mara kwa mara za kimwili kama vile kutembea upesi kwa dakika 30 au zaidi.
4.  Usinywe sana kileo. Watafiti fulani wanasema kwamba wanaume walio na ugonjwa wa kupanda kwa shinikizo la damu hawapaswi kunywa zaidi ya mililita 30 za kileo kila siku, wanawake na vilevile watu ambao si wazito sana hawapaswi kunywa zaidi ya mililita 15 za kileo.
Kileo cha mililita 30 kinalinganishwa na mililita 60 za vinywaji aina ya Spirits kama wiski & vodka, kadhalika mililita 240 za divai (Wine) au mililita 720 za pombe (Beer).

5.  Kutumia lishe yenye matunda na mboga. Kwa mfano angalau visehemu vitano kwa siku.
6.  Kula vyakula vingi vyenye potasiamu, magnesi na kalisi. Uchunguzi mbalimbali unaonyesha kwamba kula vyakula vingi vyenye potasiamu na kalisi kwaweza kupunguza shinikizo la damu.
7.  Dhibiti mfadhaiko.
8.  Acha kuvuta sigara.
9.  Dhibiti kiwango cha kolesteroli (Choresterol).
10.  Dhibiti ugonjwa wa kisukari.
11. Usitumie dawa zinazoweza kuongeza shinikizo la damu.

MWISHO

Imeandikwa na
Dk. Joachim mabula

manyandahealthy@gmail.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s