Watu 11 wamefariki dunia wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa na lori,wilayani muheza

Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi vibaya baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ”Thende Sheki” kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la mkanyageni lililopo wilayani muheza.

Ajali hiyo ilikusanya mamia ya wananchi kutoka jijini tanga,muheza na lushoto kwa ajili ya kwenda kushuhudia na kutambua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa nje katika hospitali teule ya mtakatifu augustino wilayani muheza kwa ajili ya utambuzi ambapo hadi majira ya mchana miili ya watu 9 waliokufa papo hapo katika eneo la tukio ilitambuliwa na ndugu na jamaa.

Akielezea miili na majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo,kaimu mganga mkuu wa wilaya ya muheza Dkt.Perter Shemkhai amesema watu wawili walifariki hospitali muda mchache baada ya kuletwa na kupatiwa tiba katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodai kuwa ina viashiria vya dereva wa lori hilo alikuwa amepitiwa na usingizi wakati akiwa barabarani.

Credit ITV

Follow us on
http://facebook.com/tubongetz
 http://twitter.com/tubongetz
  http://instagram.com/tubongetz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s