Mwana FA: Makampuni tusaidieni kuufanya muziki wetu uwe mkubwa, ni baada ya ushindi wa Diamond

Wasanii mbalimbali wakubwa na wadogo wameendelea kumpongeza Diamond Platnumz kwa ushindi mkubwa alioupata Jumamosi iliyopita baada ya kunyakua tuzo tatu za Channel O (CHOAMVA).

Kupitia Instagram Mwana FA ameandika jinsi anavyouchukulia kwa uzito ushindi huo wa Platnumz pamoja na ushauri wake kwa makampuni na wadau katika kuwekeza kwenye muziki.

Sawa…nilikuwa nangoja woooote mmalize ili mnisikilize sawasawa..
Sidhani kama tumeelewa vizuri haya matokeo ya Chanel O Video Music Awards safari hii..ni kuwa,nyota wetu ana awards 3,three,thalatha,hizi ️️️,na nyota wa wapopo hana yeyote..zero..nil..mikono mitupu…….
Msiliangalie juu juu hili..Africa imeona..aliyebaki haamini kuwa tuna vipaji vikubwa na vingi kuliko wapopo abaki na uchimba chumvi wake…
Makampuni,wadau,na kila aliye kwenye nafasi,bila kujali kwa ukubwa gani,tusaidieni kuufanya mziki wetu mkubwa..makampuni yanayofanya biashara zake na waTanzania yawekeze kwa wasanii wa kiTanzania..kama nchi tunahitaji hiyo kupita mnavyodhani..its a win win situation,tunaweka kwa wasanii wetu,tunakuza mziki wetu,tunatunza na kuthamini vipaji vya watu wetu na tunasaidia uchumi wetu kukua kila mmoja kwa nafasi yake..kwa namna moja ama nyingine waTanzania mnaowauzia huduma na/ama bidhaa zenu watapata kupitiwa na hizo fedha mnazozipitisha kwa wasanii wao..na nchi itapata kodi yake..sio win win??ni nini then?acheni kutorosha hela zetu,hamfanyi biashara zenu na wapopo,mnafanya na waTanzania..msichukue hela kwa waTanzania then muwape wapopo..warudishieni waTanzania hela zao,WANASTAHILI..
Anyway,nimepaniki nikaamua kufungua upande wa kichwa unaokwenda mbali zaidi ya mziki..yaishe…kwanza hata sijakula mchana,inaweza kuwa ni njaa tu…..ila mmenisikia…
Kwa Chibu,we noma mwanangu..keep going..you doing it for everybody in the industry,not just yourself..I see you..salute!”

Follow us on
Facebook: http://facebook.com/tubongetz
 Twitter: http://twitter.com/tubongetz
  Instagram: http://instagram.com/tubongetz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s