Rais JK amemteua Profesa Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Profesa Mussa Juma Assad 

Rais Jakaya Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuanzia Novemba 5, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ilisema Assad ataapishwa leo saa nne asubuhi Ikulu.

Awali, alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Asaad anachukuwa nafasi ya Ludovick Utouh aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka minane na kuagwa rasmi Septemba 20, mwaka huu.

Uzoefu

Taarifa ya Balozi Sefue, ilisema kuwa Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha, ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1988.

Akizungumzia uteuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alipongeza uteuzi wa Profesa Assad kuwa CAG, akisema kwa sababu hiyo uhakika katika uwajibikaji katika fedha za Serikali umeongezeka.

Alisema kwa kiwango cha ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma na ufisadi kilichochopo, Tanzania inahitaji sheria na kanuni madhubuti na mtu mahiri na mwadilifu wa kuzisimamia kama Profesa Asaad.

Alisema Profesa Assad anafahamika kuwa siyo mpenzi wa vyombo vya habari lakini utendaji wake bora wa kazi utajieleza wenyewe na kuwa ataisaidia ofisi hiyo kwenda hatua zaidi ya pale alipoachia Utouh.

Credit Mwanachi

Follow us on
Facebook: http://facebook.com/tubongetz
 Twitter: http://twitter.com/tubongetz
  Instagram: http://instagram.com/tubongetz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s