2014 ni mwaka wa joto kali duniani

Mwaka huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014, wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya wastani uliokuwepo muda mrefu.

Na miezi kumi na mmoja ya kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.
Utafiti mwingine uliofanywa na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu.

Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Mataifa, WMO, limeonya kuwa dunia inakabiliwa na mwaka wenye kiwango cha juu kabisa cha joto tangu rekodi zianze kuchukuliwa ambapo shirika hilo limesema, inathibitisha mwenendo wa ongezeko la joto likiendana na mabadiliko ya tabia nchi.
Shirika hilo limesema kupanda kwa viwango vya joto katika uso wa bahari vilikuwa vinasababisha mvua zisizo za kawaida katika nchi za Morocco, Uturuki na nchi za Blakan, Ulaya mashariki na kusababisha ukame mkali katika maeneo mengine duniani. Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Michel Jarraud, amesema kuongezeka kwa utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira na mgandamizo wake angani kunaisababishia dunia kutokuwa na uhakika wa hali ya hewa na hali mbaya ya baadaye.

Follow us on
Facebook: http://facebook.com/tubongetz
 Twitter: http://twitter.com/tubongetz
  Instagram: http://instagram.com/tubongetz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s