Skendo ya kurekodi mkanda wa ngono, Zari wa Diamond kwisha!

Hizo ndizo kauli zilizozagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii mara baada ya habari ya kurekodiwa video ya utupu ya mwanadada anayedaiwa kuwa mwandani mpya wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kuchapishwa gazetini nchini Uganda.

GAZETI GANI?
Gazeti la Red Pepper la Desemba 5, mwaka huu ndilo lililomponza mwanadada huyo kwa kuripoti kuvuja kwa video ya utupu ya mrembo huyo na kusababisha aonekane hafai mbele ya jamii. Wadau wengi wakaanza kuhoji kwa nini akubali kurekodiwa video hiyo wakati yeye ni mtu mzima tena mama wa watoto watatu?

VIDEO YAZUA GUMZO
Vyanzo tofauti mitandaoni vimeielezea video hiyo. Kuna ambavyo vimedai kuwa mwanadada huyo alirekodiwa ‘akijichua’ mwenyewe huku vyanzo vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai alirekodiwa akivunja amri ya sita na mpenzi wake wa zamani.

ZARI AFUNGUKA
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari mwenye maskani yake nchini Uganda na Afrika Kusini, aliandika kuwa mtu aliyevujisha video hiyo chafu alikuwa na lengo la kumharibia shoo yake anayotarajia kuifanya Desemba 18, mwaka huu inayofahamika kama Zari All White Party lakini hawatafanikiwa.

Hii ni kwa mashabiki wangu wote duniani, vyombo vya habari vya Uganda vimenichafua kwa kuingilia uhuru wangu pamoja na familia yangu ili kuniharibia na picha hizi za zamani… katika akili yangu najua kabisa picha zilizotoka leo (Ijumaa iliyopita) kwenye Gazeti la Red Pepper zimevujishwa na mtu kwa madhumuni yake binafsi.
Kimsingi sitashindwa, shoo itafanyika kama kawaida na Diamond atakuwepo kama kawaida. Niwahakikishie tu nitachukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyehusika kunichafua,” aliweka nukta Zari.

GAZETI LAKOMAA
Licha ya mwanadada huyo kudai atawafikisha kwenye mikono ya sheria wahusika wote, bado ilielezwa kuwa gazeti hilo lilizidi kukomaa na kudai wana ushahidi wa kutosha.

WABONGO SASA
Mara baada ya habari hiyo kuzagaa mitandaoni, Wabongo walilipuka kama moto wa kifuu na kuanza kutoa maoni kuhusu mrembo huyo ambapo wengi walidai ni mara mia Diamond angeendelea kuwa na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ kuliko Zari.

Mmeona sasa mtu ambaye Diamond aliona amepata kumbe si lolote si chochote, mtu mwenye akili zake atakubalije kurekodiwa video ya utupu? Kwa kweli mara mia Diamond angebaki na Wema wake ambaye hana skendo kubwa kama hii, Zari kwisha kabisa, hapa ndiyo mwisho wake, aibu ya mwaka hii,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.

MWINGINE AMTETEA
Pamoja na wadau wengi kumponda Zari na kudai ndiyo mwisho wa heshima yake, kuna mdau mwingine mtandaoni alimtetea mrembo huyo anayefanya muziki kuwa ni mwanamke jasiri na Diamond anatakiwa kuwa pamoja naye kuhakikisha wanaizima skendo hiyo, waendelee kufanya yao.

Kiukweli nimempenda Zari, anajiamini hakuona umuhimu wa kuomba radhi maana anajua ni vitu ambavyo alivifanya kabla hajakutana na Diamond,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.

TIMU WEMA VICHEKO
Wakati saga hilo likizidi kupata ‘kavareji’ mitandaoni, wafuasi wa Wema (Timu Wema) waliashiria kufurahia kitendo cha mrembo huyo kurekodiwa video hiyo ya utupu.

Safii, si alijifanya anajua kutuchukulia shemeji letu sasa limemshuka shuuu…akome,” mmoja wa memba wa Timu Wema alitupia komenti yake.

HATA HIVYO
Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, Wema ndiyo alimmwaga Diamond na si Diamond kummwaga Wema wala kumwagana!

TUJIKUMBUSHE!
Zari na Diamond wanaodaiwa kuzalisha penzi jipya hivi karibuni (project), kila kukicha wamekuwa wakinadi urafiki wao mitandaoni huku kila mmoja akionesha kumsapoti mwenzake kimuziki ambapo Desemba 18, mwaka huu wameahidi kufanya bonge la shoo nchini Uganda.

Follow us on
Facebook: http://facebook.com/tubongetz
 Twitter: http://twitter.com/tubongetz
  Instagram: http://instagram.com/tubongetz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s