Davido ampiga dongo Diamond kuwa ni ‘Jiwe lisilo na shukrani hatimaye huanguka’!

Huhitaji kujifikiria mara mbili kuamini kuwa Davido na Diamond haziivi tena kwa sasa!
Yote yalianza baada ya Davido kutweet ‘N they cheat again, Lol’ baada ya Idris kutangazwa mshindi wa Big Brother Hotshots. Tweet hiyo ikimfanya Davido atukanwe matusi ya kila aina kutoka kwa Watanzania.

Usiku huo huo, Diamond alishinda tuzo za TFA (The Future Awards) za Nigeria na kuandika:

Thanks God, we have cheated another one on The Future Awards Africa in Lagos Nigeria… #SameDay #SameNight Thank you Allah.” Ujumbe huo moja kwa moja ukaashiria kuwa jibu kwa Davido ambaye matusi kutoka Tanzania yaliendelea kumsakama.

//platform.twitter.com/widgets.js
Baadaye, Davido anayeaminika (na huo ndio ukweli) kuwa msanii aliyesaidia kumtambulisha Diamond kimataifa, aliandika ujumbe kwenye Twitter unaoshiria kumlenga Diamond.

An ungrateful stone will eventually fall… I will always be grateful to pple that have helped me climb this tall ladder of success,” alitweet Davido.

Tweet hiyo ilimaanisha: Jiwe lisilo na shukrani hatimaye huanguka… Nitakuwa mwenye shukrani siku zote kwa watu walionisaidia kuipanda ngazi ya mafanikio.

Hata hivyo naye Diamond alitumia siku ya Uhuru wa Tanganyika jana kutoa nasaha zake kuhusiana na mikwaruzano baina ya wasanii wa Afrika kwa kuandika:

Badala ya wasanii kuwa ndio mfano bora wa kuweka karibu nchi zao na kujenga Afrika yenye upendo na amani…eti wao ndio wanakua chanzo cha kutenganisha nchi zao. Namna hii kweli tutajenga Afrika? Anyway, Happy Independence day Tanzania.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s