Mchezaji avunja kanuni za kifalme kwa kumshika begani Kate Middleton akiwa na majasho

Mchezaji wa mpira wa vikapu LeBron James alivunja protokali au kuvunja kanuni za maadili ya kifalme alipomshika mabegani Kate Middleton akiwa na majasho kwenye jezi lake huku mumewe Kate, Prince William akifanya mzaha kuhusu ukubwa wa mguu wa mchezaji huyo huku wote wakiangua kicheko.

LeBron aliweka mkono wake katika bega la Kate kwake mambo yakiwa ni kawaida tu

Wengi nchini Uingereza wameandika kwenye mitandao ya kijamii wakimwambia LeBron sio vyema kuweka mkono wake kwa bega la mkewe mwanafalme hasa wakatui jezi lake likionekana kuwa na jasho jingi.

Haya yalitokea punde baada ya mechi ya mpira wa vikapu ambayo Prince William na mkewe mjamzito Kate Middleton walishuhudia mjini New York wakati wakipigwa picha za pamoja.

LeBron James, alitumbukiza mpira kwenye neti mara nyingi tu lakini inasemekana laijiweka katika hatari ya kukosa mwlaiko wa krismasi kutoka kwa familia hio ya kifalme kwa kumkumbatia begani Kate.

Prince William na Kate walipigwa picha baada ya mechi kati ya Cleveland Cavaliers mjini New York Jumanne walipkuwa wakicheza na Brooklyn Nets, ambapo walikabidhiwa jezi ya mwanao mwenye umri wa mwaka mmoja Prince George.

Lakini kamera zilipokuwa zinapigwa, James aliweka mkono wake kwenye bega la Kate na kuvunja kanuni za maadili ya kifalme, licha ya kujulikana kwa jina la mzahaha kama King James.
Baada ya tukio hilo, wawili hao walikwenda kukutana na wanamuziki mahiri duniani Jay-Z na mkewe Beyonce kupigwa picha nyingine.

Lakini je unahisi kuwa mchezaji LeBron alivunja kanuni za kifalme kwa kumsika Kate begani?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s