Hivi ndivyo ulivyo kuwa usiku wa UEFA Champions league

Hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ilimalizika usiku wa jumatano ikishuhudia michezo nane ambayo ilipigwa kwenye viwanja tofauti barani humo .

Katika michezo iliyopigwa siku hiyo Fc Barcelona walijihakikishia ushindi wa Kundi F baada ya kuwafunga mabingwa wa Ufaransa PSG kwa matokeo ya 3-0 .

PSG ndio walioanza kufunga kwenye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic bao ambalo halikudumu kwa muda mrefu kwani Lionel Messi alisawazisha .

Barca hawakuishia hapo kwani dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika walifunga bao la pili safari hii mfungaji akiwa Neymar.

Kazi katika usiku mzuri kwenye uwanja wa Nou Camp ilimalizwa na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez aliyefunga bao la tatu .

Matokeo haya yanawafanya Barcelona kufuzu kama washindi wa kundi lao huku PSG nao wakifuzu kama washindi wa pili.

Kwingineko Manchester City wakiwa ugenini kwenye mji mkuu wa Italia walifanikiwa kuwafunga As Roma 2-0 ushindi ambao umewapa tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora kama washindi wa pili kwenye kundi lao nyuma ya Bayern Munich.

City walifunga kupitia kwa Samir Nasri na Pablo Zabaleta ushindi uliowafanya wafikishe pointi nane .

Katika michezo mingineAjax Amsterdam waliwafunga Apoel Fc 4-0 , Chelsea waliwafunga Sporting Lisbon 3-1, Fc Schalke wakashinda dhidi ya NK Maribor kwa matokeo ya 1-0 , Athletic Bilbao wakawafunga Bate Borisov 2-0 na Fc Porto na Shakhtar Donetsk wakatoka sare ya 1-1.

Kwa matokeo haya timu za Barcelona , PSG , Chelsea , Schalke 04 , Bayern Munich , Manchester City , Fc Porto na Shakhtar Donetsk zimefuzu hatua ya 16 bora zikiungana na timu zilizofuzu hapo jana ambazo ni Real Madrid , Fc Basle , Atletico Madrid , Juventus , Borusia Dortmund , Arsenal , Monaco na Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora ambayo ratiba yake itapangwa jumatatu ijayo .

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s