Mapigano ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kimasai yawaibisha wazinzi waliokuwa gesti

Vijana waliokamatwa kwenye vurugu hizo.

Mapigano ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kimasai yaliyotokea hivi karibuni katika Kitongoji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani hapa yamewakurupua wazinzi waliokuwa wakifanya uchafu wao katika nyumba ya kulala wageni.

Mwanahabari wetu aliyenasa tukio hilo lililotokea Desemba 9, mwaka huu, alimshuhudia dereva wa lori ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, akitoka katika gesti maarufu eneo la Dumila akiwa na nguo ya ndani huku binti aliyekuwa akibanjuka naye akikurupuka na taulo ambapo nguo zake za ndani na mazagazaga yake alicha chumbani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mapigano hayo yaliyodumu kuanzia saa 4 asubuhi hadi 10 jioni, yaliibuka baada ya mmasai huyo kumkata mkono mkulima katika mashamba ya Kijiji cha Mteteni alipokuwa akimzuia kukata majani shambani kwake.

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya wakulima kuona mwenzao amekatwa mkono, walijikusanya na kuwavamia wafugaji hao ili kulipa kisasi.

Wamasai baada ya kuzidiwa nguvu na kundi hilo la wakulima, waliamua kukimbilia msituni ambapo baada ya kuwakosa, wakulima hao waliamua kufunga barabara kuu ya Morogoro-Dodoma inayokatiza kwenye Kitongoji cha Dumila kushinikiza serikali ya wilaya, mkoa na taifa kuwaondoa wamasai kwenye wilaya yao,” kilieleza chanzo hicho.

Wakati hayo yakiendelea ndipo vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa kutoka katika jamii ya wakulima walipoamua kuvamia gesti na nyumba za wamasai kisha kuvunja vioo vya madirisha na baadaye kuvunja mlango.

Mbali na dereva wa lori na kiburudisho chake ambacho pia hakikujulikana jina lake kukurupuka katika gesti hiyo, mwandishi wetu alishuhudia wateja wengine wakitimka wakiwa watupu huku wengine wakiwa wameshikilia nguo za ndani mkononi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s