Dereva bodaboda amchoma visu mwenzake hadi kumuua

Dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Seleman (mwenye flana) akimshambulia kwa visu mwilini dereva mwenzake  anayefahamika kwa jina la Panya Road.

DEREVA bodaboda mmoja aliyefahamika kwa jina la Seleman amedaiwa kumchoma visu mwilini dereva mwenzake wa aliyefahamika kwa jina la Panya Road na kumsababishia kifo.

Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano iliyopita asubuhi maeneo ya Tungi-Msikitini, Kigamboni, jijini Dar katika chumba ambacho Seleman alikuwa amepanga.“Inasemekana Panya Road ilikuwa kama tabia yake iliyozoeleka ya kumnyatia mwenzake akiwa katoka kidogo anaingia na kuondoka na chochote cha thamani atakachokikuta.

Bahati mbaya leo (Jumatano) Seleman alikuwa ametoka mara moja na mlango wake hakuwa ameufunga sasa aliporudi ndiyo akamkuta Panya Road akiwa ndani kwake akitaka kumuibia ndipo kasheshe lilipoanzia hapo,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa baada ya Seleman kumkuta Panya Road ndani kwake, inadaiwa aliamua kuchukua sheria mkononi ambapo alichukua kisu na kuanza kumchomachoma sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha avuje damu nyingi.

Tulisikia kelele katika chumba cha Seleman lakini kila tukipiga hodi mlango haukufunguliwa zaidi ya kelele kuongezeka. Hatukukata tamaa tuliendelea kuita mpaka Seleman akafungua mlango lakini nguo zake zilikuwa zimeloa damu,” kilisema chanzo.

Baada ya kutolewa nje Seleman, majirani waliendelea kumsihi asiendelee kumchoma mwenzake lakini hakuacha, alizidisha hadi pale walipomvaa na kumpora kisu.Hata hivyo baadaye polisi wa Kituo cha Kigamboni walipigiwa simu na kufika mara moja ambapo walimchukua Seleman na Panya Road akiwa hajitambui ambapo imedaiwa kuwa alikata roho kabla hajafikishwa hospitali.

Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya M. Kihenya kuhusiana na tukio hilo, alisema taarifa za tukio hilo hazijamfikia lakini akaahidi kulifuatilia mara moja.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s