Nikki Mbishi: Wananchi elekezeni nguvu zenu kwa wasanii wengine pia, si Diamond tu!

Rapper Nikki Mbishi ameibuka na kudai kuwataka mashabiki wa muziki wa Tanzania kuwaunga mkono wasanii wengine pia na sio Diamond au wasanii wengine wachache wanaopewa kipaumbele zaidi.

Akizungumza kwenye kipindi cha Genge cha EFM leo, Nikki Mbishi alisema wasanii wote wanahitaji kusaidiwa ili wawepo wengi wakubwa.

Hadi leo hii unataka kuniambia kuna super star mmoja Diamond na wengine wote ni washkaji zotu tu wa mitaani wanaoturusharusha tu majukwaani sio mastaa, hawana hadhi ya kuwa mastaa, mimi mwenyewe nikiwepo,? amehoji Mbishi.

Kwa wenzetu nje, msanii anakuwa label anakuja anatoa ngoma moja kesho yake staa, anaishi maisha mazuri, gari nzuri, anaendesha maisha yake vizuri na anapewa ile heshima kuwa huyu kweli ni icon. Hauoni kama itakuwa siku tukiwa na watu kama Diamond mia mbili Tanzania, na kwanini ile dhana ya utumwa Nikki Mbishi hata akawa nominated kwenye tuzo za Zanzibar, lakini nobody is going to pay attention kwa kum-support Nikki Mbishi kwa sababu ni msanii pekee!

Acha Nikki Mbishi hawa akina Peter Msechu wanakuwa nominated sometimes kwenye matuzo makubwa duniani lakini you will never hear watu wakisema jamani msupport Dabo, Mtanzania anayetuwakilisha, why Diamond only? Kwamba Diamond akiwa kwenye show basi ndo watu muache shughuli zenu mum-support? Sio hatuwezi ku- create watu kama yeye wakawa mia mbili tukiwa watu wote tunamwangalia huyo mmoja? Yule atakuja kupotea naye kwenye game ina maana watanzania kutakuwa hakuna kitu. Kama tulivyoshindwa kwenye soka hivyo hivyo na tutashindwa kwenye muziki na sisi tunachokiweza ni Big Brother.”

Kama uliikosa 411 ya leo unaweza.
https://www.hulkshare.com/embed.php?fn=7qatlr8e9vgg
Credit EFM.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s