Diamond Platnumz avunja rekodi maeneo mengi

WIKI iliyopita katika simulizi hii ya Diamond  tuliishia pale ambapo staa huyo aliongelea namna wimbo wake wa Mbagala ulivyopendwa kiasi cha kumfanya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ kumteua kuwa mburudishaji kwenye ziara za kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, mwaka 2010.Wiki hii tunaendelea…

Oktoba 2, mwaka 2010, Diamond alipata safari yake ya kwanza kabisa ambapo alikwenda jijini London, Uingereza na kufanya shoo.Mwaka 2011, Diamond alishinda Tuzo ya

Nzumari iliyotolea nchini Kenya akiwa Msanii Bora wa Kiume toka Tanzania.
Diamond aliweka rekodi ya msanii wa kwanza Bongo kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Maisha Club jijini Dar na kujaza mashabiki wengi kiasi kwamba wengine walishindwa kuingia ndani ya ukumbi huo.

AACHIA ALBAMU YA PILI
Ilikuwa Januari, 2012 Platnumz aliachia albamu yake ya pili  na kufikia rekodi ya kuwa msanii nambari wani Bongo kuuza kopi zaidi ya 1,200,000.

Mwaka huohuo,  Diamond alifanya shoo bab’kubwa iliyoitwa Diamonds are forever iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kwa kiinglio  cha shilingi 50,000. Diamond alikuwa peke yake na aliuza tiketi  zaidi 1,500.

MSANII WA KWANZA BONGO KUSHUKA UWANJANI NA CHOPA
Mei, 2012, Diamond aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufanya shoo ya nguvu na kujaza zaidi ya watu 10,000 kwa kiingilio cha 20,000 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live  huku akishuka uwanjani hapo na chopa (helikopta). Hata hivyo, Desemba 25, mwaka huu (Krismasi), Diamond atakuwepo tena ndani ya Dar Live!

AENDA ULAYA, AKAMUA
Mwaka huohuo 2012,  Diamond alifanya
ziara Ulaya ambapo alitembelea nchi kadhaa kama Italia, Uholanzi, Sweden na Ugiriki, nako alifanya shoo za nguvu.

Nyota ya 2012 ilizidi kuwa nzuri kwa Diamond kwani aliachia nyimbo mbili kwa mpigo, Nataka Kulewa na Kesho zilizoambata na video zake zenye ubora.

AWA BALOZI
Mwanzoni mwa mwaka 2013, Diamond alichaguliwa kuwa balozi wa kampuni moja ya vinywaji baridi nchini na  kufanya ziara nchi za Afrika Mashariki, Burundi, DRC, Kenya, Uganda na Rwanda na kuwa msanii wa kwanza katika nchi za ukanda huo kupiga shoo peke yake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000.

ASHINDA TUZO TENA
June 2013, Diamond alishinda tuzo mbili  za Tanzania Kili Music Awards akiwa Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Fleva na Msanii Bora  wa Kiume kwa wanamuziki wote nchini.

NUMBER ONE
Julai 2013, Diamond  aliachia singo ya Number One ambayo video yake aliifanyia jijini Capetown, Afrika Kusini na Kampuni ya Ogopa Video. Aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kuzindua video hiyo bila kiingilio ndani ya Hotel ya Serena na kuwaalika viongozi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, Diamond alifanya tukio la kihistoria ambapo alimzawadia gari aina ya Totoya FunCargo aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.

Credit GPL
Itaendelea wiki ijayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s