Licha ya kuwa Shilole amefanikiwa zaidi kwenye muziki, lakini ameweka wazi kuwa hajaitupa kabisa fani yake ya uigizaji ambayo alianza nayo kabla ya muziki.
Akizungumza kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm wakati akitambulisha wimbo wake mpya Dec.15, amesema kuwa bado anajipanga na atakuja kutoa filamu yake mpya siku za usoni.
Saizi nimejikita sana na haya mambo mengine (muziki), sio kwamba nimeacha kuigiza ila nafatutia timing, so lazima nijipange vizuri[…] so bado najipanga kiukweli kwenye sekta ya kuigiza lakini soon nitatoa filamu yangu.”
Shishi pia amezungumzia filamu aliyopanga kuitengeneza itakayoitwa ‘Shilole In Dar’.
Nitaifanyia Igunga, napenda kuizungumza kwa sababu bado sijaifanya kiukweli inaitwa Shilole in Dar, yaani kutoka Igunga hadi Dar es salaam, alikopitia kuanzia mwanzo mwisho mpaka sasa hivi anaongea hapa…kwahiyo ni true story”
Credit Clouds FM.