Video: ‘Herieth Paul’ Model wa Tanzania anayefanya kazi na Tom Ford, Calvin Klein, Armani, Cavalli na aliyekava Vogue, Elle, Glamour

Herieth Paul alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza umri wa miaka 19, December 14.
Tofauti na miaka mingi ambapo siku hiyo humkuta aidha kwao Canada au anakoishi kwa sasa jijini New York, Marekani, siku hii ilimkutia kwenye ardhi ya nchini aliyozaliwa, Tanzania.

Akiwa na umri huo, Herieth ameshafanya mambo makubwa kwenye fashion kuliko models wengi maarufu wa barani Afrika. Ameshashiriki kwenye fashion show za madesigner wakubwa duniani wakiwemo Diane von Fürstenberg, Lacoste, Tom Ford, Calvin Klein, Armani, Cavalli, 3.1 Phillip Lim na wengine.

Ameshatokea kwenye kava ya majarida kibao kama Vogue Italia, Teen Vogue na zingine, Glamour, Elle Canada, Arizona Muse, Dress to Kill, Freja Beha, Marie Claire kutaja machache tu.

Herieth alizaliwa kwenye hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alikulia Keko na kusoma shule ya msingi Chang’ombe. Mama yake aliyekuwa akifanya kazi ubalozi, alihamishiwa nchini Canada akiwa na umri wa miaka 14. “Kwanza nilitaka kuwa muigizaji,” anasema. “Nilikuwa na waangaliwa watoto wa kule nawaona kwenye TV wanacheka nikamwambia mama ‘naomba unipeleke nikawa actress’ akasema ‘okay’. Kufika pale kumbe ilikuwa agency ya modeling sio ya kuwa actress.”

Anasema pamoja na kupelekwa sehemu ambayo hakutarajia, agency hiyo iligundua ana kitu ndani yake. “Kujaribu kumbe kweli nikaweza, ni talent ambayo ilikuwa tu inside, nilikuwa kweli sijajua. Wakapiga picha wakapelekea New York, kesho yake nikaitwa.”

Alipofika New York, Herieth alianza kuishi peke yake, akiwa na miaka 14 tu na upweke ukaanza kumpa shida. “Kitu kilichonipa shida ni kuwa mbali na familia, nilikuwa mdogo sana, najipikia mwenyewe, namake sure sitaibiwa chochote, sitapigwa halafu ikiwa usiku nampigia simu mama nalia. Nilikuwa nalia yaani hakuna mtu wa kuniwekea maji ya moto, hakuna mtu wa kunipigia, hamna mtu wa kunipikia, hakuna mtu wa kunibembeleza.”

Hata hivyo Herieth anasema alivumilia tu huku pia akiendelea na shule ya Canada. “Mwalimu alikuwa ananitumia kazi kwenye computer, ikiwa siku ya mtihani narudi Canada nafanya.”

Kazi yake ya kwanza tu baada ya kuchukuliwa na agency ya Women Management ilikuwa ni Vogue Italia ambako alikutana na maisha ya kuwa model wa kimataifa ikiwemo kazi ya kupigwa picha.

“Inaonekana kama kazi rahisi lakini sio rahisi, unasimama pale lights, camera unasimama pale masaa matano hukai, huli. Mpaka wapate picha moja, wanapiga kama elfu hamsini wanatafuta moja tu.”

Jarida la Elle Canada mwaka 2012 lilimweka kwenye kava lake na kuandika kichwa cha habari ‘Naomi Move Over . Why We’re Hot For Herieth’.

“Nilijisikia vizuri kupitia kiasi. Naomi Campbell ni mtu ambaye yuko mbali sana, kazi yake anaifanya vizuri kupitia kiasi. Nilisikia kama pressure fulani ya kufika ambako yeye amefika. Lile gazeti walinifuata actually shuleni. Tukapanda treni tukaenda mji mwingine wa Canada wakapiga picha siku hiyo wakasema ni ‘cover try’ wanashoot watu wengi lakini cover yangu ikaweka. Wakasema mtu gani ambaye unampenda sana ambaye anakuinspire. Nikasema Naomi Campbell wakasema ‘unajua unafanana naye’ kipindi hicho nilikuwa na nywele bado nikasema ‘no sifanani naye, yule mzuri’ wakasema ‘kweli unafanana naye, ukiwa mkubwa kidogo utaonekana kama yeye. Basi vile wakaandika pale kama catchy phrase kwenye cover.”

Katika umri alionao na mambo aliyoyafanya, Herieth anakiri kuwa Mungu amembariki mno.

“Vitu ambavyo nimevifanya, kazi ambazo nimezifanya na umri nilionao, Mungu ananipenda sana.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s