Hakuna bifu kama ilivyo dhaniwa, Diamond Platnumz amsifia Davido, Krismasi naye yupo Dar live!

WIKI iliyopita tuliishia pale ambapo staa wa Bongo Fleva, Diamond aliachia video yake ya Number One katika uzinduzi usiyo na kiingilio alioufanya ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo pia alimzawadia gari, aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.

Wiki hii tunaendelea ambapo katika kuanika maisha yake, Diamond anasema:

ASIFU KAMPANI YA DAVIDO
“Mwezi wa 10, 2013  nilifanya kolabo na Davido (David Adedeji Adeleke) kutoka nchini Nigeria katika video ya Number One remix halafu nilifunga safari hadi Nigeria lengo likiwa ni kuangalia masoko ya muziki katika nchi za wenzetu.

“Naweza kusema wimbo wa Number One ndiyo uliweza kunitambulisha kimataifa, nilipata mashabiki kibao  na kushiriki kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo MTV Mama nchini Afrika Kusini ambapo nilipanda jukwaani na Davido. Kuna tuzo nyingine kama BET, Afrimama, MTV Europe  Channel O,” alisema Diamond.

Julai 7, mwaka huu, Diamonnd alimzawadia gari mama yake aina ya Toyota Lexus pia aliachia video mbili za Mdogomdogo iliyofanyika nchini Uingereza na Bumbum aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliyoifanyia Afrika Kusini. Video hizi anasema zilimgharimu  dola 78,000 za Marekani.

KUTUA DAR LIVE KRISMASI
Hivi karibuni, Diamond alikuwa nchini Uganda kwenye shoo ya nguvu ya mwanamuziki wa nchi hiyo, Zarina Hassan ‘Zari’ lakini amerudi Bongo haraka sana kwa sababu keshokutwa (Alhamisi) anapanda kwenye jukwaa la Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem kwa ajili ya kutoa raha ya Sikukuu ya Krismasi.

Diamond atapanda na Mzee Yusuf wa Kundi la Jahazi Modern Taarab.
Anaitwa Diamond Platnumz, mzaliwa wa Kitongoji cha Tandale kwenye Jiji la Dar es Salaam, ameweza kukitumia kipaji chake vizuri na kupata mafanikio makubwa sana. Hongera sana Diamond.

Credit GPL.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s