Uchaguzi wa mitaa, Diwani CCM anusurika kipigo kwa kuokolewa na polisi

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kigogo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Richard Chengula wiki iliyopita alipata wakati mgumu, baada ya kunusurika kupigwa na wananchi wake, kwa kile kilichodaiwa kuzuia shughuli za maendeleo.

Polisi akiwazuia wananchi wasimpige Diwani, Richard Chengula.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa tatu na nusu asubuhi wakati zoezi la upigaji kura wa serikali za mitaa likiendelea. Inadaiwa kuwa baada ya mafuriko ya mara kwa mara ya mto Tenge uliopo katika mtaa wa Mkwajuni, wananchi hao walichangishana fedha na kukodi katapila kwa ajili ya kusafisha na kuzibua maji.

Wakati shughuli hiyo ikiendelea, kwa mshangao wa wengi, diwani huyo alijitokeza na kuwakataza kuendelea na shughuli hiyo, jambo lililopingwa kwa nguvu zote na wananchi hao, ambao walimgeuzia kibao na kutaka kumshushia kipigo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuona anazidiwa nguvu, diwani huyo alikimbilia katika jengo la kiwanda cha kununua na kusaga mifupa cha Ferner Center Limited ambako aliomba hifadhi na kuwapigia simu polisi ili waje kumuokoa. Baada ya dakika chache, askari waliwasili eneo la tukio walikokuta watu wengi wakipiga kelele nje ya kiwanda hicho.

“Tumeamua kumtukana na kutaka kumpiga kwa sababu siyo mtu wa kuleta maendeleo kabisa. Yeye hata siku moja hajawahi kuleta katapila la serikali kwa ajili ya kazi hii, sasa sisi wenyewe wananchi tumechangishana halafu yeye anakuja kutuletea upuuzi, ndiye amefanya Kata yetu kuwa nyuma kimaendeleo,” alisema mwananchi mmoja kwa jazba kubwa.

Inadaiwa kuwa kutokana na kadhia hiyo, wananchi hao kwa pamoja waliungana na kuhamasishana kupiga kura za hasira na kuwapa wapinzani, ambapo mitaa miwili kati ya mitatu ya kata hiyo, ilichukuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) huku mtaa mmoja uchaguzi wake ukiahirishwa hadi ulipofanyika juzi Jumapili.

“Huyu diwani pamoja na kwamba ni bosi wangu kichama, lakini ametuudhi sana na yeye ndiyo kikwazo kikubwa cha kusababisha mitaa kuchukuliwa na vyama vya upinzani kwa sababu baada ya kutuingilia wananchi walimweleza wazi kuwa mitaa yote wanaipa upinzani na ndivyo ilivyokuwa, yaani hata wanaccm wamekasirishwa sana na kuipa kura CUF,” alisema mjumbe mmoja wa nyumba kumi ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

Diwani Chengula alikiri kukutana na mtafaruku huo akidai kuwa alikwenda eneo hilo ili kutoa ushauri wa kitaalamu lakini cha ajabu, akajikuta mambo yakimbadilikia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s