Maradhi ya utando mweupe kinywani

Ziko sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hii ya kutokea kwenye kinywa, lakini chanzo chake kikubwa ni maradhi yanayosababishwa na fangasi.

Maradhi ya fangasi ya kinywa huweza kuathiri koo pia. Vijidudu vinavyoathiri hujulikana kama oral candidiasis na wale wanaoshambulia koo huitwa oesophageal candidiasis.

Utando wa kinywa ni maradhi ni maradhi yanayosababishwa na vimelea vya fangasi aina ya hamira ambao hushambulia eneo la ndani ya kinywa na koo.
Kwa kawaida kinga ya mwili pamoja na vimelea vinavyokaa mwilini vya aina ya bacteria huzuia fangasi hawa wasiongezeke.

Inapotokea uwiano huu wa kinga ya mwili na vimelea aina ya bacteria kushindwa kuzuia ongezeko la vimelea hivyo vya fangasi ndipo hali huwa mbaya na kusababisha utando mdomoni.

Maradhi haya ni kawaida kuonekana kwa watoto wachanga. Maradhi haya hutokea kutokana na hali ya kutokuwa na uwiano sahihi kati ya kinga ya mwili wa mtoto na vimelea aina ya bacteria.

Inapotokea yakatokea kwa mtu mzima, basi mara nyingi huwa kuna viashiria hatarishi kama vile upungufu wa kinga.

Mfano ni watu wenye maradhi ya muda mrefu kama saratani, kisukari na ukimwi au mwanamke wajawazito, hali hiyo hushusha kinga zao.

Tatizo hili huwapata pia watu wanaotumia dawa kwa muda mrefu hususani dawa za vijiuasumu (antibiotic) au za maradhi yanayotibiwa  kwa muda mrefu kama vile saratani.
Kinachoweza kusababisha hali hiyo pia ni msongo wa mawazo wa muda mrefu.

Maradhi haya kwa kawaida siyo ya kuambukiza ingawa mtoto mchanga mwenye maradhi haya huweza kuyaambukiza matiti ya mama yake.

Dalili ni utando mweupe ambao huonekana kwenye kinywa eneo la ulimi na mashavuni kwa ndani. Kwenye koo huonekana kwenye kuta zake.

Mara nyingi eneo lenye rangi nyeupe huzungukwa na eneo lenye rangi nyekundu na lililovimba kidogo. Hii hutokana na mashambulizi ya fangasi.
Maeneo haya yaliyoshambuliwa huwa hayana maumivu makali lakini huweza kutoa damu kama yakiguswa au kusuguliwa.

Dalili nyingine za maradhi ni pamoja na kuonekana kwa sehemu ndogo zenye rangi nyeupe ndani ya kinywa, kupasuka kwa midomo, midomo kuongezeka ukubwa, hisia za kukwama kwa chakula kwenye koo, kuvimba kwa fizi, ladha ya chakula kubadilika na pumzi yenye kutoa harufu.

Kwa watu ambao kinga kinga ya mwili imeshuka, maradhi haya huweza kusambaa kutoka kwenye kinywa na kushuka kwenye koo la chakula mpaka kufikia kwenye tumbo.

Hii inapotokea, mgonjwa hupata maumivu wakati wa kumeza chakula.
Dalili za hatari ni mgonjwa kupata homa kali ikiambataan na kutetemeka mwili na kushindwa kabisa kumeza chakula.

Mgonjwa akifikishwa hospitali maradhi haya hutambulika kirahisi kutokana na dalili zake kuweza kutambukiwa kwa kuangalia kwa macho.

Matibabu ya maradhi haya hutegemea na kilichosababishwa. Iwapo kilichosababisha kinaweza kuepukwa au kutibika, basi nayo yataisha, kama mtu ameyapata kutokana na kuugua kisukari, ni vyema akakitubu kisukari kwanza.

Watoto wachanga hawahitaji matibabu ya aina yeyote kama dalili zitaanza kuisha kabla ya wiki nne hazijaisha.

manyandahealthy@gmail.com

Credit Manyanda Healthy.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s