Vanessa Mdee kwa mara ya kwanza amewatoa kimasomaso wasanii wa kike Bongo

MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee kwa mara ya kwanza amewatoa kimasomaso wasanii wa kike Bongo kwa kutwaa tuzo ya kimataifa za All Africa Music Awards ‘AFRIMA’ nchini Nigeria.

Akizungumza na paparazi wetu Vanessa ambaye amepata tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki alisema anawashukuru mashabiki kwa kuwa wameonesha moyo wa kumpigia kura mpaka kuwashinda wasanii wengine wa Uganda na Kenya kama vile, Wahu, Size 8, Kaz (wa Kenya) na Jackie Chandiru wa Uganda.

“Nina furaha sana kwani ni mara yangu ya kwanza kupata tuzo ya kimataifa pia nimewatoa kimasomaso wasanii wenzangu wa kike, kikubwa nawashukuru mashabiki wangu kwa kunipa sapoti kubwa ya kunipigia kura, ninawaahidi kwamba nitaendelea kufanya muziki mzuri ambao wataupenda na kuwa mwanamuziki wa kimataifa zaidi,” alisema Vanessa.

Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Desemba 27 huko Lagos, Nigeria pia msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ alipata tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki huku msanii Peter Msechu ambaye naye alikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho akikosa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s