Wema Sepetu afunga mwaka kwa kilio, Amtaja Van Vicker kama chanzo cha kuachana na Diamond Platnumz

Wakati pazia la mwaka 2014 likifungwa leo, mama la mama, Wema Sepetu ‘Madam’ ameuaga mwaka huo kwa staili ya kilio cha nguvu.

Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam akilia huku akibembelezwa na shost yake Aunt Ezekiel.

NI KWENYE SHOO YAKE

Tukio hilo lililozua maswali mengi bila majibu, lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, mwaka huu kwenye shoo ya Madam ya kuuaga mwaka 2014 (Say Good Bye To 2014) iliyofanyika katika Klabu 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar.

SHOO KWANZA

Kabla ya kukutwa na kisanga hicho kwenye shoo hiyo ambayo Madam aliiandaa chini ya Kampuni yake ya Endless Fame, shoo mbalimbali kutoka wasanii kibao wa Bongo Fleva kama Barnaba, Izo Business, Bob Junior na wengine wengi zilihusika kisha baadaye Wema alipanda jukwaani na kumtambulisha msanii wake mpya ajulikanaye kwa jina la Ally Luna.

TUJIUNGE NAYE

Ally Luna atasimamiwa shughuli zote za kimuziki na mimi chini ya kampuni yangu Endless Fame, na atapata huduma zote za muhimu kama inavyofanyika kwa msanii wangu wa zamani, Mirrow,” alisikika Wema.

KILIO SASA

Mara baada ya shoo hiyo iliyoambatana na bethidei ya mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kumalizika, Wema alikutwa na mapaparazi nje ya ukumbi huo akiangua kilio cha nguvu ambacho hakikujulikana moja kwa moja ni cha nini.

MAUMIVU YA MAPENZI?

Hata hivyo mnyetishaji mmoja aliwatonya waandishi wetu kuwa huenda Wema analia na maumivu ya mapenzi hususan akifikiria gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa kwenye siku yake ya kuzaliwa na kusababisha aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitilie shaka.
Huenda huyu ana maumivu yake ya mapenzi si bure, pengine ni hili gari alilokuja nalo ndilo linamtesa vilevile,” kilisema chanzo hicho.

AUNT AMBEMBELEZA DK 13

Mapaparazi wetu walimshuhudia shosti wa  wa damu wa Madam, mwigizaji Aunt Ezekiel akitumia dakika 13 kumbembeleza staa huyo ambaye juzikati alikuwa nchini Ghana kurekodi sinema na mwigizaji kiwango nchini humo, Van Vicker.

ASEMA KABANWA NA MLANGO

Ili kutaka kujua sababu za Madam kuangua kilio kwa muda mrefu, baada ya kunyamaza, mapaparazi wetu walimvaa Wema na kumuuliza kulikoni? Msikie alivyofunguka:
Nimeumia  kwenye mlango wa gari langu baada ya mtu kufunga mlango wa nyuma na kunibana vidole vyangu vya mkono maana nilipata maumivu nahisi kama vimevunjika maana hapa siwezi hata kushika kitu kabisa hata gari kuendesha siwezi najuta kushikilia mlango wa gari yangu.

WATU WAPINGA

Licha ya majibu hayo, watu waliosikia jibu hilo hawakuamini ambapo walidai haiwezekani kwa mtu mzima kama yeye kuangua kilio kiasi hicho kwa muda mrefu.
Hataki tu kuanika ukweli, kuna jambo linamtesa hataki tu kuliweka wazi,” alisikika mmbeya mmoja aliyekuwa eneo hilo.

AMTAJA VAN VICKER KUWAACHANISHA NA DIAMOND

Katika hatua nyingine, Wema alipoulizwa sababu za kumwagana na Diamond, alisema pamoja na sababu nyingine, Van Vicker alihusika kuwafanya wamwagane na mpenzi wake huyo waliyedumu kwenye penzi zito lililokuwa gumzo kila kona ya Bongo.
Kuna vitu vingi vimechangia lakini Van pia amechangia, alianza ku-like picha zangu, nikamwambia Dai (Diamond), akaniambia achana naye, baadaye tulibadilishana namba, tukawa tunawasilianaIlipofika wakati amenitaka tufanye kazi pamoja, nilipomwambia Diamond ndiyo matatizo yalipoanzia hadi kufikia hatua ya kuachana,” aliweka nukta Wema.

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s