Kwahizi picha yawezekana Jux na Vanessa Mdee wathibitisha kuwa ni wapenzi!

Kwa mara kibao Vanessa Mdee na Jux wamekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi licha ya kuonesha dalili nyingi ya kuwa ni item.

Lakini huenda mastaa hao wanataka kuufanya uhusiano wao official kwa mwaka 2015. Vee Money ametoa hint kuhusu uwezekano wa wawili hao kuwa pamoja kwenye picha aliyoweka Instagram leo.

A1 since Day 1

A post shared by VeeMoney 🇹🇿 (@vanessamdee) on

“A1 since Day 1,” ameandika Vanessa kwenye picha hiyo ya black and white inayoonesha wazi kuwa wapo kwenye dimbwi la mahaba mazito.

Naye Jux amepost picha akiwa na Vee na kuandika:

I know I’m late but better late than never. Nataka kuwashukuru wote kwa Upendo wenu mlionyesha Mwaka wa 2014, nawa ahidi burudani zaidi na mziki mzuri zaidi this year and hopefully through Gods grace in the years to come. God bless your 2015. I got to share mine with Miss Award Winner #AfricanBoy #InGodITrust.”

Akijibu swali la kama ana uhusiano wa kimahaba na muimbaji huyo wa ‘Nitasubiri’, Vanessa aliwahi kujibu,”Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu.”

Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile nyimbo ya Monefere. Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano Nahareel asingekuwa na Aika basi nahisi na yeye pia wangesema hivyo. Ila sio hivyo wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,” Vee aliiambia Bongo5.

Naye Jux alikuwa na majibu yale yale pindi swali hilo lilipokuwa likitupwa kwake. “No ni mshikhaji wangu tu, tunafanya naye kazi, kuna tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki na Stamina, Mo Music ni kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia toafuti ndio maana imekuwa hivyo,” alisema Jux.

Hata hivyo alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke.
Ni msichana mzuri, mwonekano wake mzuri, she is smart, yeah she is a wife material, yuko vizuri, lakini na mimi tumeendana sana tabia zetu kama washikaji. Sema nipo naye karibu na kwa sababu mimi sionekanagi na wasichana wengi ndio maana imekuwa hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa sasa hivi ni mapema, vyote anapanga Mungu,” alisisitiza Jux.

Credit Bongo 5.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s