Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amsema Diamond kuwa hana akili timamu, Kisa issue ya kumzalia mtoto

Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.

MAHOJIANO

Katika mahojiano maalum ya hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Runinga ya GlobalTV Online chenye makao yake makuu ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge, Dar, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha kupata mtoto.

Alisema kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka nao kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na uvumba.

MZOZO MKUBWA

Hata hivyo, madai hayo ya Diamond yalizua mzozo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku warembo hao wakipigwa za uso hivyo kutafuta namna ya kujitetea.“Hao akina…(wanatajwa warembo wa Diamond) watakuwa wana matatizo ya uzazi siyo bure.

“Ndiyo maana Dangote (Diamond) ameona bora aende kwa Zari (msanii wa Uganda, Zarinah Hassan) ambaye tayari ana mwanga wa kuzaa (ana watoto watatu),” ilisomeka sehemu ya maoni juu ya madai hayo ya Diamond kwenye Mtandao wa Instagram.

SIKIA MADAI YA DIAMOND

Diamond alifunguka: “Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”

JOKATE AJIBU MAPIGO

Kufuatia tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa staa huyo wa Ngoma ya Ntampata Wapi inayokimbiza kwa sasa.
Jokate alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.

JOJO ASHUKA NA MISTARI

“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kwenda kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,” alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.

WEMA HATAKI MALUMBANO

Ukiacha Jokate na Wema ambaye naye aliwekwa kwenye kapu moja la kuchenga kumzalia, hakutaka kumjibu Diamond kwa kuwa hataki malumbano au makuu na mtu.

PENNY ALISHAJIBU

Pia jamaa huyo alimzungumzia aliyekuwa mwandani wake mwingine, Penniel Mwingilwa ‘Penny’ kuwa yeye alitoa mimba zake mbili kwa visingio tofauti.Katika majibu yake kupitia gazeti tumbo moja na hili, Risasi Jumamosi, toleo la wiki iliyopita, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.

NENO LA MHARIRI

Baada ya kila mmoja kupata nafasi ya kufunguka kivyake, ni vyema sasa malumbano yakaisha na kuuanza mwaka 2015 kwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa jumla.

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s