Vanessa Mdee awashauri wasanii kutumia vyema mitandao ya kijamii

Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro za mwaka jana kwenye kipengele cha wimbo bora wa R&B, Vanessa Mdee, amewashauri wasanii wa Tanzania kuwa makini katika kile wanachokiandika kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Vanessa amedai kuwa wasanii wengi wanatakiwa kujitambua kuwa wao ni bidhaa iliyopo sokoni muda wote na heshima yao inapimwa kwa kile wanachokiandika kwenye mitandao ya kijamii na jinsi wanavyowasiliana na mashabiki wao.

Kwa sasa Instagram ndio mtandao unaotumiwa zaidi na mastaa wa Tanzania.

Hivi karibuni Vanessa Mdee alishinda tuzo za muziki za All Africa Music Awards 2014 zilizotolewa jijini Lagos, Nigeria kwenye kipengele cha muimbaji bora wa kike kutoka Afrika Mashariki. Vanessa anatarajia kuachia album yake ya kwanza ‘Money Mondays’ baadaye mwaka huu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s