Diva wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ akwaa skendo ya kuiba mume wa mtu

WAKATI diva wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ akielezwa kuwa mambo yake hivi sasa yako kwenye mstari kwa kusajili kampuni yake ya mambo ya sinema, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Pamela ameibuka na kumtaka muigizaji huyo kuacha kumfuata mume wake.

Mwanamama huyo, anayefanya kazi ‘nzuri’ katika shirika moja kubwa nchini, aliliambia gazeti hili kuwa Kajala, amekuwa akitembea na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Tanaluza ambaye kwa sasa yuko ndani katika gereza la Keko kwa kosa ambalo alikataa kulitaja.

“Jamani namtahadharisha Kajala, asije kunikuta pale, patakuwa hapatoshi, yeye si hodari wa kwenda kuangalia waume za watu, awe na haya, aende Ukonga akamuangalie mumewe, ushauri wa bure nampa,” alisema Pamela kwa jazba.

Alisema anazo taarifa kuwa Kajala alikuwa akitembea na mumewe kabla hajapatwa na matatizo na baada ya kupelekwa Keko gerezani, amekuwa akienda hapo kwa kujifichaficha, kitu ambacho alisema siyo kizuri kwa sasa, kwani anaweza kumsababishia mumewe matatizo zaidi.

“Huyo ni mume wangu, ananihitaji kwa hali na mali sasa hivi, nisije nikaacha kwenda kwa ajili ya Kajala, kama aliwahi kumpangishia nyumba ya kifahari na kumnunulia gari, ni huko huko, sasa hivi anahitaji kuwa na mimi mkewe, kwanini yeye asiende kwa mume wake na yeye si amefungwa?,” alihoji Pamela.

Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mke, gazeti hili liliingia mtaani kwa nguvu kumsaka Kay, ambaye mume wake, Faraja Augustino amefungwa jela miaka saba kwa kosa la utakatishaji fedha na kufanikiwa kumpata kupitia simu yake ya mkononi.

“Mimi mbona simjui huyo mwanaume, wala sijawahi kufika huko keko, kama anatafuta umaarufu kupitia jina langu aseme, asinisingizie,” alisema Kajala baada ya kusomewa mashtaka yake, majibu ambayo licha ya kuyaheshimu, lakini gazeti hili linaendelea na uchunguzi wake ili kubaini ukweli zaidi.

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s