Zarinah Hassan ‘Zari the BossLady’ alala kwa mama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’, Sinza-Mori jijini Dar.

Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Zari alipata fursa ya kupiga ‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea Diamond.

“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.

“Awali, Diamond alitaka akamlaze hotelini lakini mtoto wa kike akakataa, akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe, Diamond akasema ruksa mama,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.

“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s