Hii ndiyo baruwa ya wazi kwa Afande Sele juu ya ukweli kumsaidia Daz Baba

Barua hii ikiwa imechapishwa na tovuti ya GPL kupitia kipengele chao cha ‘Za Chembe, Lazima UKAE‘ inamuhusu msanii Afande Sele kuhusianan na ukweli ambao utamsaidia msanii ambaye kwa sasa amebobea kwenye ulevi wa kupindukia Daz baba. Kama ilivyo andikwa isome nawewe pia hapa chini.

SELEMANI Msindi, ndiye msanii wangu bora kabisa wa tungo za kiume, zinazopeleka ujumbe moja kwa moja pasipo mafumbo na kama itabidi liwe fumbo, kwa wanazuoni, ni rahisi mno kujua mlengwa.

Wengi wanamfahamu kama Afande Sele, kijana wa pale Morogoro ambaye wakati f’lani akitafuta maisha, aliwahi kujaribu kupata ajira katika Jeshi la Polisi, chanzo hasa cha jina lake hili la kisanii. Kati ya wasanii wakubwa ninaowafahamu kwa karibu kupitia kazi zao, huyu naye yumo!

Kitu kimoja kizuri ni kwamba Afande Sele anajua vizuri lugha ya Kiswahili, ndiyo maana tungo zake zimekuwa kielelezo cha msanii makini anayejua nini anaimba, kwa ajili ya nani na kwa wakati gani.

Haikuwa ajabu alipotwaa taji la Mfalme wa Rhymes katika shindano la pekee kuwahi kufanyika nchini. Nimefanya naye kazi kwa ukaribu, ninamfahamu kwa kiwango cha kuridhisha. Ingawa ni mtu makini akiwa nyuma ya mic, nje ya fani Afande anabaki kuwa mswahili tu kama tulivyo waswahili wote, anacheka na kila mmoja na anawang’ong’a kila wakimpa kisogo!

Ingawa mimi ni shabiki wa kweli wa Afande, mtu ninayemkubali sana, huenda kwa sababu ya kuwa naye karibu kikazi, nimegundua tatizo lake moja la msingi, kuna wakati, kwa sababu anazozijua mwenyewe, huamua kuikwepa nafsi yake inayojulikana na kujivika asiyokuwa nayo.

Kwa hili, nimewahi kutofautiana naye mara kadhaa na ninachoshukuru, hakikuwahi kuharibu ukaribu wetu. Afande anasema asichotenda na anatenda asichosema! Wote tunajua, wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya wamejitumbukiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya (Cocaine na Heroin) na wapo rafiki na ndugu zetu wamepoteza maisha kwa kuhusishwa na jambo hili, ingawa enzi za uhai wao, walikuwa wakikataa katakata kujihusisha nalo.

Nimewahi kusema mara kadhaa, watu hawawezi kumzushia mtu kitu kisichofanana na ukweli. Kwa mfano, tunao watu, ambao ni marafiki zetu, ndugu zetu na hata wafanyakazi wenzetu, wanatajwa kuwa ni mashoga, walevi, wezi na kadhalika. Hatuwezi kuamini moja kwa moja, lakini pia hatuwezi kupuuza. Kwa nini watajwe wao na siyo wengine?

Hatuna ushahidi, lakini utapuuza vipi unaposikia kila siku watu wanawataja Banzastone, Msafiri Diouf, Chid Benz, TID, Lord Eyez, Ray C na wengine kuwa wanakula ‘sembe’?Juzi, nimesoma mahali, mshkaji wangu Afande Sele akimtetea Daz Baba, yule mkali kutoka Kundi la Daz Nundaz, aliyetamba na vibao vingi vikiwemo Umbo Namba Nane, Elimu Dunia na kadhalika, kwamba kudhoofika kwake mwili hakutokani na utumiaji wa madawa ya kulevya, bali ni unywaji pombe uliopitiliza.

Ninamfahamu Daz Baba na ninajua Afande na Daz Nundaz ni washkaji. Anachofanya ni kujaribu kupooza sauti isiyokoma, inayopaza kuwa bwa’ mdogo anakula unga. Kama nilivyosema mwanzo, hatuna ushahidi, lakini kwa nini tupuuze sauti hii, inayotolewa na watu wanaomfahamu?

Kumsaidia Daz Baba na wengine wanaotajwa ni kuwaambia ukweli kuwa wanapoteza mwelekeo. Tuwaambie kuwa wanachokifanya sasa ni ujanja wa kizamani, ambao umewapoteza watoto wengi wa Kariakoo, Magomeni, Kinondoni, Mwananyamala, Ilala na Temeke, ambao leo hii wamekuwa ombaomba kwa watu ambao wakati wanaingia mjini kutafuta maisha, wao waliwaita wakuja!
Kwa hiyo ningetegemea Afande Sele, siku moja aachie kibao kinachowataja washkaji zake wabwia unga, akiwataka waache, kwa ajili ya Tanzania salama!

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s