Huu hapa ukweli kuhusiana na ujauzito ‘Chibu Dangote’ Diamond Platnumz alio mpachika Zari The BossLady

BAADA ya kufunguka kuwa zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ wamegoma kumzalia, habari ya mjini kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni kwamba anadaiwa kumdunga mimba mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’.

CHANZO CHAVUJISHA MCHAPO

Wiki mbili zilizopita, chanzo kilicho karibu na Diamond kiliwalipenyezea mchapo mapaparazi wetu kuwa uhusiano wa Zari mwenye maskani yake Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ na jamaa huyo tayari umejibu hivyo mashabiki wa mastaa hao wategemee ujio wa uzao wa wawili hao.

Hivi habari ya Zari kuwa mjamzito mnayo? Mbona iko wazi na Diamond amefurahi sana maana si unajua tena alihangaika sana kupata mtoto kwa Wema, Jokate na Penny wote wakamzingua? Sasa habari ya mjini ndiyo hiyo,” kilidai chanzo hicho huku kikiomba chondechonde kistiriwe jina.

DIAMOND ATHIBITISHA KIAINA

Wakati wanahabari wetu wakiendelea kuchimba undani wa habari hiyo, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, Diamond alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram iliyoashiria kwamba anathibitisha yale yaliyovujishwa na chanzo chetu kuwa yana ukweli.

PICHA ILIKUWAJE?

Picha hiyo aliyoitupia Diamond ilikuwa ikimuonesha mtoto wa kike, Zari akiwa amelala kwenye mapaja ya Diamond ikiwa imeambatanishwa na picha ya ‘Ultrasound’ kuonesha tumbo la Zari lina kiumbe kilichoanza kurutubishwa.

ASINDISIKIZA NA UJUMBE

Chini ya picha hiyo, Diamond alisindikiza na na ujumbe ulisomeka hivi:
I can not wait to have you on my hand…# Chibu_Junior.”
(Siwezi kusubiri kukubeba mikononi mwangu Chibu Mdogo)

AITOA MTANDAONI

Katika hali ya kushangaza, wakati wapenda ubuyu wachache wakiwa ‘wameshaiiba’ picha hiyo mtandaoni, Diamond aliitoa fasta ikidaiwa kuwa alishauriwa kufanya hivyo.
Atakuwa kashauriwa aitoe maana si unajua tena Wabongo wangeanza kumshambulia, akaona bora atoe fasta,” aliandika mmoja wa wadau wa Diamond mtandaoni.

ZARI NAYE ATUPIA

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Uganda, mara baada ya Diamond kuposti picha hiyo, Zari naye aliichukua na ‘kui-repost’ katika akaunti yake kisha na yeye kuitoa baada ya muda mfupi.

YAWA GUMZO UGANDA

Baada tu ya Zari kuposti na kuitoa picha hiyo, vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vikijadili picha hiyo na kufanya mastaa hao wawe gumzo nchini humo huku wadau mbalimbali wakitoa maoni yao.
Tunampongeza Diamond kwa kuunganisha undugu kati ya Tanzania na Uganda, kama wamekubaliana wazae tu hakuna shida,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki mtandaoni juu ya ishu hiyo.

DIAMOND ANASEMAJE?

Wanahabari wetu walimuibukia kwa zaidi ya mara tano Diamond nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar lakini hakuwepo, baadaye alipatikana kwenye simu na kujibu kwa kifupi:
We kama umeona kwenye akaunti yangu unauliza nini tena?

MTU WA KARIBU

Ili kuzidi kuchimba ukweli wa habari hiyo, wanahabari wetu walimvutia waya mtu wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda kuanika jina gazetini lakini akakiri kuwa Zari ana mimba ya Diamond.
Mbona kitambo tu, Diamond alivumilia kwa muda mrefu lakini jana usiku (Jumanne kuamkia Jumatano) ndiyo akaamua kuweka picha kisha akaitoa,” alidai mtu huyo wa karibu na Diamond.

KUMBUKUMBU

Kabla ya habari hiyo ya mimba ya Zari, huko nyuma Diamond aliwahi kuambiwa hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke lakini mwenyewe alifafanua kwamba wachumba wake wote ‘aliobanjuka’ nao kwa nyakati tofauti, waligoma kumzalia kwa kile alichokiita ni kupenda ‘utoto wa mjini.’

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s