Yapate hapa matokeo ya ‘NECTA’ mtihani wa kidato cha pili mwaka 2014 yaliyo toka 2015

Matokeo ya wanafunzi wa kidato cha pili mwaka 2014 yametoka rasmi jana tarehe 17th Jan, 2015 ambapo inaonyesha masoma ya sayansi yamekuwa ni kizaa zaa kuliko masomo ya sana.

Bofya hapa kuyapata Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2014.

……………………………………………………………………
……………………………………………………………………

Sayansi ni ‘shida’ kidato cha pili

Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani la taifa,Dk Charles Msonde

Juhudi za Serikali kuinua ufaulu wa masomo ya sayansi katika elimu ya sekondari sasa zitakuwa zimepata picha halisi ya hali ilivyo baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha pili kuonyesha ufaulu mdogo katika masomo hayo na mwanafunzi mmoja tu akipata alama zote katika somo la bailojia.

Hata hivyo, matokeo ya kidato cha pili yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), yanaonyesha ufaulu mkubwa kwa matokeo ya masomo yote kwa jumla.

Kati ya watahiniwa 453,191 waliosajiliwa kufanya mtihani huo Novemba 24 hadi Desemba 5 mwaka jana, ni watahiniwa 405,204 sawa na asilimia 89.0 waliofanya mtihani na watahiniwa 47,987 sawa na asilimia 10.60 hawakufanya.

Kati ya watahiniwa hao, wasichana walikuwa 233,834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana 219,357 sawa na asilimia 48.40.

Akitangaza matokeo hayo jana jijini hapa, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema: “Somo ambalo limefanya vibaya zaidi ni hisabati… Walifanya wanafunzi 381,973 na waliofaulu ni 69,332 sawa na asilimia 18.15, sayansi ya kilimo waliofanya walikuwa 18,946 na waliofaulu ni 6,526 sawa na asilimia 34.45.”

Alifafanua kuwa jumla ya watahiniwa 375,434, sawa na asilimia 92.66 ya waliofanya mtihani mwaka jana, wamepata alama zinazowawezesha kuendelea na masomo ya sekondari ya kidato cha tatu.

“Kati yao wasichana ni 195,328 sawa na asilimia 92.63 na wavulana ni 180,106, sawa na asilimia 92.69. Watahiniwa 29,770 sawa na asilimia 7.34 wamepata alama ambazo baraza limeona ni bora wakarudia darasa,” alisema Dk Msonde.

Alisema: “Mwaka 2013 watahiniwa waliopata alama za kuendelea na kidato cha tatu walikuwa 422,446 sawa na asilimia 89.34 ya watahiniwa 472,833 ya waliofanya mtihani huo.”

Pia, alieleza kuwa katika mtihani wa kemia, waliofanya mtihani walikuwa 399,725 na waliofaulu ni 153,613, sawa na asilimia 38.43. Waliofanya somo la fizikia walikuwa 398,502 na waliofaulu ni 154,318 sawa na asilimia 38.72 wakati somo la biashara walikuwa 78,331, waliofaulu ni 33,411 sawa na asilimia 42.65.

Alimtaja Sophia Boneka kutoka Sekondari ya Heritage Dar es Salaam kuwa ndiye aliyepata alama 100 katika somo la biolojia kati ya watahiniwa 400,105, huku akishika nafasi ya 10 kati ya 381,973 kwenye somo la hisabati.

Dk Msonde alisema somo la uraia aliyepata alama 100 ni mmoja kati ya watahiniwa 378,139 ambaye ni Martine Jackson kutoka Shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema: “Tatizo la masomo haya kufanya vibaya linaweza kuangaliwa kwa mapana zaidi, labda kuna matatizo kwa walimu wanaowafundisha au wanafunzi wenyewe hivyo ni jukumu la wadau kulitazama hili.”

“Watahiniwa wamefaulu vizuri katika masomo ya uraia, historia, Kiswahili na Kiingereza kwa asilimia 84.0 ya watahiniwa waliofanya mtihani pia somo la historia likiongoza kwa wanafunzi kufanya vizuri zaidi kati ya masomo yote baada ya watahiniwa 361,698 kati ya 398,732 kufanya vizuri, hiyo ikiwa ni asilimia 90.71 walifaulu.”

“Somo lililofuatia ni Kiswahili ambalo lilikuwa na watahiniwa 398,831 na waliofaulu ni 339,351, sawa na asilimia 85.09, wakati somo la Kiingereza kati ya watahiniwa 400,934, waliofaulu ni 341,134, sawa na asilimia 85.08,” alisema.

Credit Mwananchi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s