Jinsi ya Kufanya Mazoezi kwa wasichana wadogo

Kufanya mazoezi kwa wasichana wadogo ni hitaji la msingi, hasa ikizingatiwa katika umri waliokuwa nao mabadiliko mengi hutokea mwilini mwao.

Ongezeko la mwili la ghafla ni miongoni mwa mabadiliko hayo.
Hili mara nyingi hutegemeana na tabia ya ulaji ovyo wanaokuwa nao wengi.
Mazoezi yana uwezo mkubwa ya kuwasiadia kuweka miili yao sawa na hata kuondoa katika hali ya kuongezeka. Kama wewe ni mmoja wao na ungependa kufanya mazoezi hayo, fuata dondoo hizi ili ufanikishe lengo lako.

1. KUJINYOOSHA

Hili ni zoezi la msingi katika mpango mzima wa ufanyaji mazoezi. Unashauriwa kufanya aina hii ya zoezi kama baada ya program yako. Zoezi hili husaidia kumkinga mfanyaji mazoezi dhidi. Pia husaidia kujenga misuli.

2. RUSHA RUSHA MWILI WAKO

Baada ya kufanya “strech” , fanya mazoezi ya kuruka ruka kwa muda wa dakika 10 hadi 15. Mazoezi hayo yanaweza kuwa ya kucheza zumba, kukimbia, kuruka kamba, kupanda ngazi ama kuendesha baiskeli, mazoezi haya yana sifa ya kukuongezea uwezo wa kuunguza mafuta mwilini.

3. PATA MAFUNZO YA KUNYANYUA VITU VIZITO

Wengi hudhani kuwa kunyanyua vitu vizito kunaeza kukufanya uote vitonge kwenye mikono. Dhana hiyo haina ukweli wowote, unyanyaji wa vitu vizito utasaidia kuimarisha tu misuli yako ya mwili na kukuacha ukiwa mkakamavu.

4. WAHUSISHE RAFIKI ZAKO

Fanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yako. Wahusishe na rafiki zako wa karibu. Hii itakusaidia kukuoa hamasa ya kufanya mazoezi pia wewe mwenyewe.

Credit Manyanda Healthy

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s