Zari Hassan kufunga ndoa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, "Asema hakuna umri maalumu wa Kuoa au Kuolewa"!

WAKATI mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ akiwa nchini India kwa matibabu ya tatizo la kiafya linalodaiwa kuwa ni kupooza, hapa Bongo dalili za Diamond na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au The Boss Lady kufunga ndoa zinanukia.

Chanzo makini kimeliambia Ijumaa Wikienda kwamba, licha ya mama Diamond kupelekwa India Januari 27, mwaka huu na msafara wa watu wawili, nyuma, Zari alitua Bongo tangu Januari 30, mwaka huu lengo kubwa likiwa kumuuguza mama mkwe wake huyo.

ATUA DAR, AENDA SINZA-MORI

Chanzo kikazidi kuweka wazi kuwa mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Diamond alimpokea na kwenda naye nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar bila kumwambia kama mama yake amepelekwa India kwa matibabu.
Diamond alikwenda kumpokea Zari lakini hakumwambia kama mama yake amekimbizwa India kwa matibabu na yeye (Zari) alikuja kwa lengo la kumuuguza mama mkwe wake,” kilisema chanzo.

BAADA YA KUMKOSA MAMA MKWE

Habari zaidi zilisema kuwa, walipofika nyumbani na Zari kuambiwa mama Diamond amepelekwa India, aliumia sana na kumlaumu mpenzi wake huyo kwa nini hakumwambia kuhusu safari ya mama tangu walipokutana uwanja wa  ndege.

YAISHA, DIAMOND AMPELEKA ZARI KWENYE UJENZI

Baada ya kuwekana sawa kuhusu usiri wa safari ya mama’ke, Diamond alimchukua Zari na kumpeleka kwenye nyumba yake anayoijenga Mbezi-Beach, Dar kwa lengo la kumuonesha sehemu ya mali zake ambapo ilisemekana nyota huyo wa Uganda aliipenda ramani ya nyumba  hiyo.

ZARI AGOMA TENA KULALA HOTELINI

Katika siku za hivi karibuni, tuliwahi kuandika kuwa Zari alilala kwa mama Diamond, akapika na kupakua ambapo mawifi zake walimsifia.
Hata katika ujio wake wa Juni 30, mwaka huu, mrembo huyo mwenye utajiri mkubwa aligoma kwenda kulala hotelini na kumwambia Diamond atalala naye nyumbani kwao, Sinza-Mori.

ZARI AANZA KUBADILI DINI?

Zari ni Mkristo wa Kanisa la Born Again ambalo ni la kiroho nchini Uganda. Aliingia kwenye imani hiyo baada kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi kama Biblia inavyotaka lakini kwa kuwa na Diamond kuna dalili za kuanza kubadili imani ili kutimiza mipango ya ndoa.
“Ukiachia kwenda kwenye nyumba hiyo ya Mbezi pia Diamond ameshaanza kumfundisha Zari baadhi ya mambo ya kidini,” kilisema chanzo.

Ijumaa iliyopita ambayo kiimani, Diamond hupenda kuvaa mavazi ya Kiarabu ambayo hutafsirika ni ya Kiislam, Zari naye alitupia vazi la baibui ili kwenda sawasawa na mwandani wake huyo.

WAENDA SONGEA WOTE

Wakati Ijumaa Wikienda likijiandaa kwenda mitamboni, habari za moto ni safari ya Diamond kwenda mjini Songea ambapo ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Diamond alikwenda kwa ajili ya shoo ya sherehe za Chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 38 tangu kuasisiwa kwake. Sherehe hizo zilifanyika kwenye Uwanja wa Majimaji jana.

ZARI KWAPANI

Habari za uhakika ni kwamba, katika safari hiyo, Diamond alimuweka Zari kwapani na kwenda naye kwa lengo la kumpa kampani.

DIAMOND: KILA KITU KINA WAKATI WAKE

Ijumaa Wikienda lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu ambapo awali alikiri mama yake kupelekwa India kwa matibabu. Kuhusu Zari kubadili dini, kuvaa hijabu na kufunga ndoa, alisema: “Mbona mna maswali sana jamani, kila kitu kina wakati wake.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s