Mtalaka wa Isha Mashauzi, Jumanne Hassan ‘Tevez’ asimulia alivyo teswa na kudhalilishwa nchini Afrika Kusini

EXCLUSIVE! Kile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani Nkongo ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kuteswa na kudhalilishwa nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!

Kwa mara ya kwanza Gazeti Pendwa la Amani Tanzania limeweza kuzungumza na Tevez kwa dakika arobaini na tano kutokea nchini humo ambako anauguza majeraha.

KWANZA SIKU YA TUKIO

Kabla Tevez hajasimulia kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu kukumbuka kuwa, tukio hilo ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es Salaam, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa zikimuonesha akiwa amefungwa kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu na majeraha kadhaa.

AMANI LAMSAKA

Kwa vile habari za tukio hilo ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari bila kupata balansi (uwiano) na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini kumsaka mhanga huyo usiku na mchana.

MSIKIE SASA

Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:
“Kusema ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo) wanalitafsiri tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu mzigo wa mtu, ndiyo maana niliteswa! Si kweli.”

UKWELI NI UPI?

“Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
“Huyu bwana inaonekana  ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.
“Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu.”

ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI

 “Katika mateso yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi milioni 22) na Landi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000) zikiwemo simu zangu mbili aina ya Sumsung na Nokia ambayo nilikuwa naitumia sana kuwasiliana na watu wangu muhimu.”

HAIKUWA KAZI RAHISI

Tevez akazungumzia jinsi jamaa walivyomkamata: “Jamaa siku wananiteka usiku kiukweli nilipambana nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na kunifunga kamba. Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa wengi na walikuwa wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya kunipiga na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo nikakuta wamenifunga kamba.”

KINACHOKUUMA NINI?

“Tukio linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha amekaa jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia sana lakini nimemwachia Mungu.”

KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA

Tevez: “Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si kweli kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama hicho zaidi ya kunichoma na pasi.
“Nimesikia wengine wanasema nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi niko safi na hali yangu ya kiafya inaendelea vizuri.”

SABA WAMEKAMATWA

Tevez tena: “Nashukuru sana serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka sasa ninapoongea na wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.
“Jana (Jumatatu) walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kunishambulia na kupora fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani baada ya siku 7, ingawa nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa Polisi Central ya huku kwa ajili ya mimi kuwatambua zaidi.”

BONGO LINI TEVEZ?

“Bongo natarajia kurudi Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu yatakuwa kwenye mstari ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi wetu ili nijue kama ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza kunisaidia kama kiongozi wangu.”

HALI YAKO KWA SASA

“Kusema ukweli naendelea vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila hili la pasi mgongoni ndiyo  linasumbua kwa mbali, lakini naamini litakaa sawasawa.”

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s