Ujauzito alio nao Zari Hassan ambao umeshaanza kujitokeza hadharani wamfurahisha mama Diamond

SIKU chache baada ya kuvuja kwa picha zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.

Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.

Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.

“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond, asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema mama Wema.
Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayehiheshimu kwa sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.

“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume gani amuoe lakini nahitaji mtu mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe ndio anaweza kuwa baba wa familia la sivyo inakuwa ni mambo ya kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa Diamond.”

Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli hiyo ya mama Wema, simu yake iliita bila kupokelewa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia picha ya Zari huku akizungushia duara tumboni na kuandika; ‘kileee kinaanza kumharibia mtu mavazi.’

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s