Kwanini Mke wa mtu na au ‘girlfriend’ wa mtu awe wa watu!

Nazungumza na wanawake ambao tayari wamekwishaolewa. Kwa takwimu zisizo rasmi sana, kadiri miaka inavyozidi kwenda ndivyo idadi ya wanawake wanaosaliti inavyoongezeka kwa kasi ya ajabu.

Kwa sasa ndoa nyingi zimegeuza fasheni, hakuna ugumu tena mke wa mtu kuwa mke wa watu. Mwanamke ana mumewe lakini si ajabu kusikia ana wanaume wengine kulingana na mazingira yanayomzunguka.

Anaweza kuchepuka na muuza genge, rafiki wa mumewe kama si bosi wake ofisini. Ukichunguza kwa makini mtu huyo, hawezi kuwa na sababu ya msingi lakini zaidi ni kwamba atakwambia, ‘amejikuta tu amechepuka.’

Wapo ambao wanaweza kuwa wamechangiwa na waume zao kwa namna moja au nyingine lakini pia wapo ambao matatizo yao si ya msingi. Nayaita si ya msingi kwani tunaweza kuyaepuka kama mhusika akiamua. Tujifunze pamoja baadhi ya mambo yenyewe:

KUJITAMBUA

Kujitambua ni jambo la msingi. Kabla hujaingia kwenye ndoa inawezekana ukawa kuna vitu ulikuwa unavifanya kwa mazoea lakini ukishaingia lazima utambue kwamba upo kwenye taasisi ya watu wanaoheshimika.
Tambua kwamba ndoa si lelemama. Tabia zile ulizokuwa ukifanya na marafiki zako, ukaribu ule unapaswa kuwa na mipaka sasa. Jifunze kupitia wake za watu waliokutangulia jinsi wanavyoheshimu ndoa zao.
Ukiruhusu maisha uliyokuwa ukiishi kabla ya kuolewa ndiyo ukaishi wakati wa ndoa utafeli maana marafiki ambao hawajaolewa, wana aina yao ya kuishi. Hawawezi kukushauri vizuri, hawajui raha wala chungu ya ndoa.

LUGHA

Ukishaingia kwenye ndoa unapaswa kuwa na lugha ya ‘mke wa mtu’. Matamshi yako yanapaswa kuwa na busara. Tumia lugha nzuri kwa mumeo hata kwa watu wanaokuzunguka. Ukitumia lugha vibaya ni rahisi kuruhusu mianya ya kuchepuka.

Wanaume wengi wanapomuona mke wa mtu ana lugha ya masihara kila wakati, haupo ‘serious’ na mazungumzo yako ni ya kupenda vitu vya matusi huwa ni rahisi sana kukufuata. Ni rahisi kukusalimia na kukuongelesha mada za aina yako na kuweza kukuteka akili.

Kuwa serious katika mazungumzo yako. Kama kuna kitu kinachokukutanisha na mwanaume mwingine nenda kwenye pointi moja kwa moja mueleze ukiwa unamaanisha juu ya kile kilichokupeleka kwake na si vinginevyo.

MAVAZI

Ukishakuwa mke wa mtu suala la mavazi ni la kuzingatia. Ili uheshimike lazima ujiheshimu kwanza mwenyewe. Vaa mavazi ya heshima ambayo yanasitiri mwili wako. Simaanishi usipendeze, hapana. Pendeza lakini vazi liwe na heshima, lisikuache nusu utupu.

Vazi lisikubane sana kiasi cha kukuonesha umbo lako lilivyo. Ukiruhusu mavazi ya aina hiyo maana yake ni kwamba unatoa mwanya kwa watu kukutamani.

Nafasi hiyo anapaswa kuwa nayo mumeo pekee. Kila mmoja anatambua maumbile ya mtu yanavyoweza kuwa kivutio kikubwa cha matamanio.

Mke wa mtu anapovaa vazi la namna hiyo, dhahiri anaonekana hajiheshimu. Kwa lugha nyepesi ni kwamba anaonesha kwamba anahitaji kutongozwa. Kwa anayejiheshimu, ni dhahiri atatunza utu wake, atatunza heshima yake katika jamii.

Anayejiheshimu hawezi kuvaa vazi ambalo litamsababishia usumbufu barabarani pia vazi ambalo haliwezi kumtofautisha na machangudoa wanaojiuza barabarani. Lazima kuwe na tofauti kati ya mke wa mtu na changudoa.

MIKAO

Mke wa mtu unapaswa kukaa na kujisitiri maungo yako hususan eneo ambalo lina wanaume tofauti na mumeo. Unapoinama kuokota kitu sehemu ambayo mpo na mumeo tu ni tofauti na utakavyoinama ukiwa na watu tofauti.
 Ukaaji wako unapaswa kuwa  na hekima kadiri uwezavyo. Usiruhusu sehemu ya mwili wako ikawa wazi.  Iwe ni kwenye gari au mahali popote, mwili wako uwe na thamani kwa mumeo tu.

Credit GPL
Itaendelea wiki ijayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s