Matonya amaliza tofauti na uongozi uliokuwa ukimsimamia

Muimbaji wa muziki aliyewahi kutamba na nyimbo kibao ukiwemo ‘Anita’, Matonya amemaliza tofauti na uongozi uliokuwa ukisimamia kazi zake.

Staa huyo amekiri kuwa kuvunja mkataba na kampuni hiyo iitwayo 360 ya nchini Kenya ni sababu kubwa iliyomfanya hivi karibuni asipate mafanikio kwenye muziki wake.

Kwa muda mrefu vitu vilikuwa haviendi sawa kwa sababu usimamizi wangu wa muziki na maisha yangu vilikuwa ni vitu viwili tofauti sasa ilikuwa nikijaribu kujikita kwenye muziki upande wa pili wa maisha mambo yalikuwa yananiendea mrama kidogo ndio maana nilikuwa nikiachia kazi zinashindwa kufanya vizuri,” amesema Matonya.

Menejimenti yangu niliyokuwa nafanya nayo kazi jijini Nairobi imerudi sasa hivi Dar es Salaam kwa sababu nisingeweza kufanya kazi mbili pekee yangu lazima tupate menejimenti ili kila kitu kiende sawa. Nashukuru imerejea salama sasa hivi makazi yake ni jijini Dar es Salaam 360 ndio kampuni inayosimamia kazi zangu tena sasa hivi kuanzia ngoma ya Sembule na zitakazofuata’’ aliongeza Matonya.

Matonya anatarajia kuachia wimbo mpya aliowashirikisha Vanessa Mdee na Rich Mavoko.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s