Hatimaye Q Chillah amezijibu tuhuma za TID aliyedai kuwa muimbaji huyo aliondoka Top Band sababu ya tamaa

Hatimaye Q Chillah amezijibu tuhuma kutoka kwa swahiba wake wa zamani TID aliyedai kuwa muimbaji huyo aliondoka Top Band sababu ya tamaa

Chillah alikuwa akijibu kauli ya TID aliyoisema kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds FM alipokuwa akisimulia sababu za wawili hao kushika kila mtu njia yake.

Kupitia 255 kwenye kipindi cha XXLm Clouds FM, Q Chillah amedai kuchukizwa na kauli aliyoitoa TID anayodai ni ya uongo.

Katika kumbukumbu yangu mimi ninachokumbuka ni kwamba mhindi alitoa milioni kumi ya ile album,” alisema Chillah. “Ilikuwa kama advance halafu tunamdai hela nyingine. Mimi nilikuwa nimesafiri nimeenda Mombasa. My only mistake nikumwambia TID ‘nenda kachukue ile hela kwa mhindi nikiwa na imani kwamba ni hela ndogo hawezi kuitolea macho amefanya biashara nyingi. Alivyokwenda kule, mhindi akanipigia simu mimi nikatoa go ahead ‘haina tatizo mimi nachelewa kurudi lakini hela umaweza ukampatia tu’

Sasa unajua hela ni hela, hela ni ibiLisi kijana alikuwa na mambo mengi akaingia tamaa akaniambia kuna milioni tatu imetoka nini halafu kwanza na mimi nimechukua tatu halafu kuna nne nyingine itatoka kwahiyo kachukua zile mbili zangu na mbili zake zikawa nne kwahiyo akawa na kama milioni 7. Mimi narudi baada ya wiki moja nikamwambia inabidi tupande ndege twende Dubai tukachukue vyombo mimi na wewe. Baadaye nikapiga hesabu kibinadamu na kiungwana nikaona tukipanda ndege watu wawili cost itakuwa nyingi hoteli na gharama nyingine nikamwambia kwanini wewe usiende una experience na band tayari,” amesimulia msanii huyo.

“Basi tumepanga vizuri namkuta asubuhi anakula bata tu. Mimi nikasema huyu si mnyama angekuwa kwenye ndege sasa hivi? Mbona yupo hapa? Mtu wa pembeni msichana, girlfriend wake akanitonya akaniambia ‘sikiliza TID akiwa na hela anakuwa kama jini anabadilika na hana ubinadamu’. Nikamwambia ‘mimi sijamzoea katika style hiyo huyu ni kama brother nimempa uongozi na nimempa madaraka naamini kabisa tutaongozana vizuri’. Kwahiyo TID kumbe ile hela kaila kaifanyia mambo mengine kaongezea kanunua gari.

Mimi nilivyorudi kwanza nilimfuata mama yake na kaka zake nikawaambia nikija mara ya pili nitakuwa na defender halafu nimtamharibia huyu jamaa sasa kaka zake ‘ooh bwana unajua TID sijui mtoto wa Kinondoni’, nikamwambia ‘mimi sitaki kujua anaishi wapi, mimi mwenyewe mtoto wa jua yaAni ‘Sun of the Sun’, no mother, no father nimezaliwa na jua.”

Walivyosikia nakuja na polisi wakaanza negotiation. Hata hivyo hawakutoa hiyo hela yote wanayotakiwa kutoa. Walichokifanya wakajipiga piga wakaja wakatoa milioni moja na nusu. Kwahiyo nilivyoiangalia katoa 1.5 na hiyo nyingine iliyobaki nikaona maskini tu, hiyo hela itamsaidia mbele.”

Kufuatia hatua hiyo, Q Chillah amesema hawezi kukaa tena na TID na kufanya naye kazi pamoja kwakuwa ameonesha si mtu mwema.

I am with another new brand, na ni band kubwa kuliko yeye anavyofikiria, afanye kitu Top Band irudi. Mimi sioni anachokifanya. Q Chillah amerudi kwa sababu ya kufanya kazi zake, Q Chillah atafanya kazi na akina Diamond, akina Alikiba, nitafanya kazi na wasanii ambao wana focus na future yao sio wasanii ambao wako tayari kuwachokoza wasanii wenzao kwaajili ya kupata kiki,” amesisitiza.

Siamini kabisa TiD anaongea nini. Mwambie mdudu hataki hayo unayoongea, mwambie nimekasikirika kusikia anaongea vitu ambavyo havina maana. Na hata kuvuta unga watu wote tumeshaacha sasa hivi. Tufanye vitu vya msingi ana watoto ana baba ana mama na aache kwanza ngada na arudi kwenye muziki kama mimi nilivyorudi na For You. Aache hizo habari. Aachane kabisa na mambo ya unga, arudi akiri, awe mwanadamu kama wanadamu wengine. Unaitwaje mnyama wakati wewe binadamu? Mwambie sasa Mzee Mugabe kashafanya mEngi kuliko yeye. Amuulizie Mugabe ni nani duniani halafu ataambiwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s