Taharuki yakumba Jiji la Tanga Polisi wakipambana na majambazi mapango ya Amboni

Tanga. Hali tete na taharuki imezuka katika Jiji la Tanga kuanzia jana baada ya kusikika milio na mabomu na risasi zilizokuwa zikirushwa wakati vikosi vya jeshi la polisi na JWTZ vikishambuliana na kundi linalodaiwa kuwa ni la majambazi.

Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga 

Milio hiyo imesababisha baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Karasha Amboni Jijini Tanga  kulazimika kuhama makazi kusalimisha uhai wao huku askari sita wa jeshi la wananchi (JWTZ) na wa polisi wakidaiwa kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga leo Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja amesema kuwa hiyo ilikuwa ni oparesheni ya ushirikiano wa Polisi na jeshi, JWTZ lengo likiwa ni kudhibiti uhalifu nchini.

Baada ya askari kufika mapangoni, kundi la majambazi lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,  askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.

Shuhuda mmoja ambaye ni mkazi wa eneo hilo, Rehema Juma (34) amesema yeye na mwenzake walilazimika kuhama kwenye nyumba zao kukimbia mapigano hayo kwa kuhofia maisha yao

Kilichosababisha tuhame ni milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona helikopta ikirandaranda tukapata hofu kubwa… hatuwezi tena kutoka kwenye nyumba zetu,” amesema Rehema Juma ambaye  yeye na watoto wake watatu wamelazimika kuhifadhiwa kwa ndugu zake mtaa wa Amboni.

Credit Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s