Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samwel Nyalandu amezijibu tetesi juu ya mahusiano yake na Aunt Ezekiel

Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu na mkewe Faraja Kotta wamejibu tetesi kuwa mheshimiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.

Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu akiwa na mkewe Faraja Kotta.

Awali tetesi hizo zilieleza kwamba Nyalandu na Aunt walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Kwa mujibu wa Nyalandu ambaye ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais mwaka huu, hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwa kuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu.
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina dili kabisa.

Waziri Nyalandu(kushoto) akiwa na Aunt Ezekiel Marekani.

“Hata anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza.

“Nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunt Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndiyo hiyohiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.

“Tumekutana naye akiwa mwalikwa pamoja na maDJ wengine wa Bongo Fleva katika tukio lenye watu wengi ambao ni Watanzania waishio Marekani.

“Nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwa hiyo kwanza katika hali hiyo ya kuwa Amerika (Marekani) atakuwa aliniona kwa saa moja kwenye ule mkutano.
 “Lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye,” alisema Nyalandu pembeni akiwa na mkewe.

Credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s