Blandina Chagula ‘‘Johari’’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘’Ray’

STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’ bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu.

Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke.

Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtafutaji,” alisema Johari.

Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi mapenzi yao yalikuwa ni ya ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ na wala si ndoa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s