Kuhusiana na Ommy Dimpoz kukataliwa kuingia Marekani na kurudisha Tanzania bila kufanya show, Msikilize hapa akielezea

Miongoni mwa stori zilizochukua headline kwenye radio mbalimbali, hata kwenye magazeti ni kuhusiana na msanii wa Ommy Dimpoz kuzuiliwa kuingia Marekani na kurudishwa Tanzania bila kufanya show zake.

Kupitia Amplifaya ya Clouds FM Ommy Dimpoz ame amplify na kusema;

…Mimi hata mwenye hizo habari zimenishangaza na kilichonishangaza zaidi stori jinsi zilivyokuja na zilizovumishwa sijui zimekuja vipi kimenishangaza zaidi au unakuta hata mtu ni professional, watangazaji, Waandishi,wengine  mtu aandika tu stori au anaongelea stori kwa maana unatengeneza stori kwa kusikia kitu ambacho hauna ushahidi wala haujamsikia mhusika pengine hata kuongea na management yangu, au lakini hata kuongelea ile kuhusu mhusika maana meneja wangu aliniambia ameulizwa imekuaje akawajibu kwamba Ommy ame ni text anarudi leo kwa hiyo yeye atakuwa na majibu yote lakini unakuta stori tu zinaongelewa ambapo hata mimi mwenyewe sijasikilizwa kitu gani kimetokea..”

Kilichotokea ni kwamba mimi nilitoka hapa nikaenda mpaka Amsterdam na Amsterdam nilikuwa na connect flight kutoka Amsterdam kwenda detroit na detroit kwenda Vegas kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss flight ya connect Amsterdam kwenda detroit kwa hiyo ikabidi ni rebook booking yangu ili nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas kwa hiyo nikakosa connection ya kwenda detroit nikapata connection nyingine ya kupitia Minnesota nilivyofika kule wakati nimefika airport ndege ambayo nilipata connection na hii ya pili ikawa tayari ilikuwa imenichelewesha kwasababu ilikuwa inatakiwa inifikishe siku ya show  sasa  pale kukawa na tatizo kule watu wa venue siku ambayo waliokuwa wameongea nao” Alizidi kuelezea Ommy Diampoz.

Kwa hiyo ikabidi waongee kuwa msanii amechelewa lakini tunaomba event tufanye siku nyingine lakini wale jamaa wakakataa wakasema haiwezekani na lengo ilikuwa mimi ni perform kwenye hiyo weekend ya ruby kwa hiyo kutokana na mazingira hayo ikabidi wale watu wa immigration unajua siku zote ukifika ile ni nchi unavyoingia siku zote lazima kuna maswali ya security pale lazima uulizwe, unajua watu hawajui kitu kimoja kwamba kupata visa sio ndio kuingia kwenye nchi ya mtu kwamba ukifika nchi yoyote hata sisi tunaenda South Africa naona ni nchi ambayo tunaingia bila visa ukifika airport lazima uulizwe unakuja kufanya nini, unakaa siku ngapi, kwa hiyo nchi zote utaratibu ndio huo kwa hiyo katika pale kuulizwa nikawambia naenda Las Vegas kwenye show, kwa hiyo mara nyingi unajua wa marekani ni watu  wakutaka kujiridhisha au  hata hapa Tanzania  wageni wanakuja unaweza ukamuona Mzungu, Mhindi, Mwarabu, mtu mweusi  akifika pale kwenye passport control lazima wahusika wa hapo airport wajiridhishe pengine  hata wapige simu kwa huyo mwenyeji wako, kwahiyo wakapiga simu kule kwa  watu wa event pamoja na sehemu ya  Venue kwa hiyo watu wa Venue wakaambiwa kulitakiwa kuwe na show ila msanii hakufika kwa hiyo wakabidi waongee na promote akasema tumeisongeza kwasababu msanii amechelewa amemiss flight sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo lilikuwa uje kwenye hii show na show tayari umeshaimiss kwasababu ya matatizo ambayo sisi hatutakiwa kuyajua yamesababishwa na nini  wakasema kwamba lakini hapa inaonesha una show nyingine New york tarehe 21 nikawaambia ndio nilikuwa ninayo ila nilipanga nikitoka Las Vegas naelekea huko”

 Ommy Dimpoz akizidi kufafanua tukio lilivyokuwa.

Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion  yangu nilikuwa nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary , kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo itabidi nirudi nyumbani  kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye show, na kama  ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani  kwa hiyo nasubiri tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida. 

Ommy Dimpoz alipo ulizwa ilikuwaje mpaka unamiss Flight? Alikuwa na haya ya kusema.

Unajua kumiss flight kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani  na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama mule uwanja unataka watu  wanatangaza  kwasababu ilishawahi kunitokea mara nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii tangazo lolote nimekaa  angani kama almost masaa tisa nafikiri nane kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka.

Kuhusiana na habari kuwa Ommy Dimpozb aligeuzia hapo hapo Air Port haya ndiyo aliyo sema kuhusiana na hilo.

Waliniweka Hotel kwasababu hiyo flight ilikuwa ni ya siku inayofata ambayo ni jioni  mpaka zile ndege zinavyotoka huku zifike Amsterdam, zifike pale kwa hiyo ilikua ni siku inayofata…” 

Sikiliza mahojiano hapa:

http://www.hulkshare.com/embed.php?fn=fqx05z8921hc Credit Millard Ayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s