Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo CBE akamatwa kwa kudaiwa ‘kufoji’ saini ya benki ya wanachuo na kuchota shilingi M 31

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Ramadhan Kirungi amejikuta akiwa korokoroni ya Kituo cha Polisi cha Daraja la Salenda jijini Dar baada ya kudaiwa ‘kufoji’ saini ya benki ya wanachuo na kuchota shilingi milioni 31.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Ramadhan Kirungi.

Kwa mujibu wa chanzo makini, wizi huo unadaiwa kubainika baada ya makamu wake, Godfrey Modest kutumwa benki kwa ajili ya kutoa fedha ambazo cheki yake ilishasainiwa.“Yule makamu aliporudi chuoni alimweleza mhusika, akashagaa sana na hakuamini kilichotokea ndipo walipoamua kumkamata rais huyo.

“Walipokwenda kumkagua kwake walimkuta na shilingi milioni 16.5 keshi zilizosalia zikiwa zimefungwa katika mafungu matatu,” kilisema chanzo chetu kikiomba hifadhi ya jina lake.

Baada ya habari hizo kutua kwenye Gazeti la Amani, mapaparazi wetu walimtafuta msemaji wa chuo hicho, Leonidas Tibanga ambaye alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa hatua zimechukuliwa na mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi huku uchunguzi zaidi ukifanyika.“Ni kweli wizo huo umetokea na hivi ninavyozungumza na wewe, mtuhumiwa yupo polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea,” alisema Tibanga.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s