Ommy Dimpoz aamua kumuanika mpenzi wake ili kupunguza usumbufu kutoka kwa wasichana

Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake ‘Achia boy’ amefunguka na kusema kuwa ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ili kupunguza usumbufu kutoka kwa watoto wa kike.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio, Ommy Dimpoz alidai kuwa kufanya hivyo ni kupunguza kasi ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakimsumbua na kumtaka kimapenzi.

“Unajua saizi nimeamua kumuweka wazi mpenzi wangu ili wajue yupo na kupunguza usumbufu kwa watoto wa kike ambao wanadhani labda niko single, japo yupo mbali lakini kufanya hivyo inasaidia” alisema Ommy Dimpoz.

Mbali na hilo Ommy Dimpoz alisema mpenzi wake huyo kwa sasa anasomea udaktari nchini uingereza na kudai ni mtu wa Afrika Mashariki.

EATV

Advertisements

Hiki ndicho chanza cha kifo cha Muigizaji Mohamed ‘Kinyambe’ Abdalah

Taarifa za kifo cha Muigizaji Mohamed ‘Kinyambe’ Abdalah, zilianza kusambaa kwa kasi kuanzia jana kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa mmoja wa viongozi wa chama cha wachekeshaji Tanzania, Mkono amesema Kinyambe amekutwa na umauti katika hospitali kuu ya mkoa wa Mbeya. Ambapo amedai Kinyambe alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na Uvimbe Tumboni.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amiin.

Mahakama imeiamuru tiGo kuwalipa AY na Mwana FA Sh2 bilioni

Hatimae Mahakama ya hakimu mkazi Ilala imeiamuru kampuni ya mawasiliano Tigo, kuwalipa shilingi bilioni 2.18 marapa AY na Mwana FA, kwa kosa la kutumia kazi zao bila ridhaa.

Mwanasheria Albeto Msando ambaye ndiye amewasimamia wasanii hao katika kesi hiyo, aliwahi kuposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa mahakamani hapo.

Gazeti la kiingereza la The Citizen imeandika kuhusiana na hukumu hiyo hii leo,

A court has awarded two Tanzanian musicians Sh2.18 billion in special damages in a landmark ruling that could set a precedent in the application of the copyright law in the country.

The huge award was won by Bongo flava artistes Ambwene Yessaya “AY” and Hamisi Mwinjuma “MwanaFA” who had sued mobile phone company MIC Tanzania (Tigo), for unauthorised use of their music as caller tunes. A caller tune is a tone that is in the form of music that is heard by a person making a call as they wait for the person being called to answer the phone.

Ilala Senior Resident Magistrate Juma Hassan granted the award on April 11 after a four-year court battle between the parties. The award also includes a separate Sh25 million in general damages.

News of the fine against Tigo only came to light this week on Tuesday when the firm went to the High Court to block the execution of the award pending its appeal. History in the copyright field would be made should the High Court uphold the judgement by the Ilala District Court.

MwanaFA said it was time those who had in the past taken the basic copyright laws for granted realised that things have changed. “This is a key moment in copyright in Tanzania. This is something that has been happening for quite a long time now mainly because of lack of knowledge and maybe because of the costs associated with such cases,” he said.

He added: “Nobody is supposed to use your work without your permission or agreement and if at all he has benefited then he is supposed to share with you according to the price tag you have set for your work.” The mobile network operator has, however, filed for a stay of execution and has appealed against the judgment and decree for payment at the High Court. The appeal was initially set to be heard on Tue

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee. Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa.Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua.

Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika Instagram. Mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014. Wakati Instagram ilipoanza ,ilikuwa eneo la kukarabati na kusambaza picha,kampuni hiyo ilieleza.

Miaka mitano baadaye,ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video. Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe.

Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita ,instagram iliambia Newbeat. Tulitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.

https://www.facebook.com/plugins/video.php?href=https%3A%2F%2Fwww.facebook.com%2Finstagram%2Fvideos%2F1009033745849136%2F&show_text=0&width=560

Je, unazijua sifa za mwanaume anayefaa kuwa mwenza wako?

Je, unazijua sifa za mwanaume anayekufaa kuwa mwenza wako? Hili limekuwa swali gumu kwa wanawake wengi ambao wamekuwa wakijiuliza watawezaje kuwafahamu au kumfahamu mwanaume f’lani kama ana sifa za kuwa mpenzi wake? Mwanaume anayekufaa katika uhusiano wa kimapenzi lazima awe na sifa zifuatazo;

AWE CHAGUO LAKO

Ni lazima mwanaume unayetaka au unayempenda awe mpenzi wako, awe na sifa kubwa ya wewe mwenyewe kumpenda, kumridhia na siyo kumpenda kwa sababu au shinikizo f’lani.

MWENYE KUJIAMINI

Mwanamke anapokuwa na mwanaume anayejiamini, anaamini yupo salama zaidi. Hata kama kuna lolote linaloweza kutokea wakiwa wote basi mwanamke hatakuwa na woga kwa sababu tu anaamini yupo na mwanaume mwenye kujiamini ambaye atakuwa kinga au mtetezi wake.

MWENYE UAMUZI

Mwanaume mwenye uamuzi ndiye anayekufaa kwa ajili ya kujenga uhusiano makini na ulio bora. Yule mwenye uwezo wa kusema jambo na kulisimamia. Awe mtu mwenye msimamo na asiyetetereka kwa jambo lolote linaloweza kumyumbisha katika uhusiano wake, kwa sababu yeye ndiye aliyeamua kupenda basi hayuko tayari kusikiliza maneno ya pembeni kwa sababu anaamini katika fikra zake.

ASIWE MVIVU

Ili kuhakikisha kuwa familia au uhusiano wako hauyumbi, mwanaume asiyekuwa mvivu ndiye anayekufaa.

Awe mtu ambaye anajituma ili kudumisha penzi na hata familia yake. Uvivu ninaouzungumzia hapa ni ule wa kimajukumu ya kutafuta fedha na anapokuwa faragha.
shutterstock-couple-huggingANAYETUNZA SIRI

Katika uhusiano wako kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kutunza siri za ndani hata kama mtakuwa mmekoseana au kuhitilafiana. Awe tayari kuvumilia jambo hilo moyoni mwake. Kama ukiona amelitoa nje basi ujue limemzidi uwezo, ndiyo maana kuna wakati mtu akitaka kukwambia jambo anakuuliza ‘je, una kifua?’

Kuna mambo mengi sana nyuma ya uhusiano ambayo mengine hayastahili kumwambia kila mtu hivyo lazima mwanaume wako awe mtunza siri.

ASIYEPAYUKA

Uhusiano wowote una migongano kama ambavyo kazi zote zina changamoto katika utendaji wake. Kwenye uhusiano, unapaswa uchague mwanaume asiye na tabia ya kupayuka mnapokuwa mmekosana. Tabia ya kupayuka kiasi cha kuwafanya hata majirani wajue jambo mnalogombania haifai.